Mtangazaji wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani wa Radio Times, Hadija Shaibu ‘Dida’.
*****
MTANGAZAJI wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani kinachorushwa kupitia Radio Times, Hadija Shaibu ‘Dida’ amefunguka kuwa kamwe hawezi kufanya kazi Ikulu kutokana na vimini anavyovitinga.Akizungumza na Amani, Dida, alisema kuwa anafurahia sana kazi anayofanya kwa sababu inamruhusu kuvaa nguo yoyote anayojisikia vikiwemo vimini.
“Kufanya kazi Ikulu ningeshindwa kwani kuvaa nguo ni kwa sheria, huwezi kujivalia tu, kazi yangu nipo huru naweza kuvaa kitu chochote kile nikajisikia nina amani, lakini Ikulu lazima utinge koti na kuchomekea,”
alisema Dida.
0 comments:
Post a Comment