Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili New York, Marekani. Kulia Mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi akifuatiwa na Mama Upendo Manongi Septemba 16, 2014
*****
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini usiku wa jana, Jumatatu, Septemba 15, 2014, kuanza ziara ya wiki mbili katika Marekani ambapo atahutubia Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN General Assembly) New York. Mbali na kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Rais Kikwete pia atahudhuria mikutano muhimu katika mji mkuu wa Marekani, Washington, D.C.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakilakiwa na maofisa mbalimbali wa Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa baada ya kuwasili New York, Marekani, Septemba 16, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakilakiwa na maofisa mbalimbali wa Tanzania baada ya kuwasili New York, Marekani, Septemba 16, 2014.
PICHA NA IKULU
0 comments:
Post a Comment