Kinda wa mashetani wekundu, Adnan Januzaj alipiga 'hat-trick', jana usiku
ADNAN Januzaj ameanza kumkuna kocha Louis van Gaal ili amujumuishe katika kikosi kitakachoikabili Leicester City wikiendi hii baada ya kuifungia mabao matatu 'hat-trick' Manchester United ikishinda 3-0 dhidi ya Sunderland katika michuano ya vijana chini ya miaka 21 (U 21).
Januzaj alifunga magoli hayo mbele ya Van Gaal aliyeambatana na mke wake kipenzi.
Mwishoni mwa wili iliyopita,nyota huyo kinda raia wa Ubelgiji alicheza dakika nane katika ushindi wa 4-0 dhidi ya QPR.
Januzaj atakabiliwa na changamoto ya namba Old Trafford msimu huu kufuatia kutua kwa Di Maria, Ander Herrera na Radamel Falcao - lakini akicheza mbele ya Van Gaal jana, alionesha kipaji cha hali ya juu.
Adnan Januzaj akifunga goli na kuufanya ubao usomeke 4-0 , kipa wa Sunderland, Maksymilian Stryjek alishindwa kabisa kumzuia kinda huyu mwenye kiu kubwa ya mafanikio.
Anderson akimpongeza Adnan Januzaj baada ya kufunga goli safi
Louis van Gaal na mke wake Truus waliitazama mechi kati ya Manchester United dhidi ya Sunderland iliyopigwa uwanja wa Old Trafford
Makocha wasaidizi wa Man United, Stuivenberg na Ryan Giggs nao walikuwepo
0 comments:
Post a Comment