MIAKA kadhaa imepita tangu kundi la Wanaume TMK livunjike na kuzaa makundi mawili ya Wanaume Family na Wanaume Halisi ambayo kwa kipindi cha nyuma yalionekana kuwa na uhasama.
Rapper/mwimbaji mkongwe wa TMK, Juma Nature amezungumza na tovuti ya Times Fm kuhusu uwezekano wa kuipata ladha mchanganyiko ya collabo kati ya wasanii wa makundi hayo mawili.
“Inawezekana hiyo ni mipango. Hauwezi kusema kwamba kitu fulani kwamba kitafanyika tu, hapana. Hiyo ni mipango tu.” Juma Nature ameiambia tovuti ya Times Fm.
“Inategemea kazi zenu zinaendaenda vipi, mko karibu? Kwa sababu kila mmoja sasa hivi ana familia yake ujue. Huwezi kumchukua huyu kwenye familia yake ukamwambia tufanye hili wakati kila mmoja ana kundi lake.” Ameongoza.
Amefafanua kuwa hakuna mwiko wowote kati ya wasanii wa kundi lake kufanya kazi na wasanii wa kundi lolote lile.
“Hakuna mwiko wowote yaani, kazi zinafanyika tu kwa kuwa wote wanajua sanaa na wote ni watu wa watu.”
Chanzo: Times fm
0 comments:
Post a Comment