![TMF](http://www.ibn-tv.com/wp-content/uploads/2012/02/TMF-300x211.jpg)
MKUTANO NA
WAANDISHI WOTE MKOA WA MBEYA
Salamu
nyingi kutoka Tanzania Media Fund.
Napenda
kuchukua nafasi hii kuwaalika rasmi waandishi wote wa habari jijini Mbeya
kwenye mkutano wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania, maarufu kama TMF
utakaofanyika tarehe 22 Agosti 2014 kwenye ukumbi wa GR Hotel, Soweto jijini
Mbeya.
Mkutano
utaanza saa mbili na nusu.
Lengo la ujio wa timu ya TMF jijini Mbeya inatokana na ukweli kwamba
kumekuwa na maombi machache sana ya ruzuku ya vijijini kutoka kwa waandishi wa
mkoa wenu. Kwa maana hiyo basi, TMF inakuja na utaratibu wake wa 'Ideation'
ambao humpa nafasi mwandishi wa habari mmoja mmoja kuelezea wazo lake la habari
za kiuchunguzi kwa magwiji wa TMF (mentors) ambao hulitafakari na kuamua kama
linastahili kupewa ruzuku ya TMF.
Hivyo basi, TMF inakuomba uwataarifu waandishi wote mkoani kwako, pamoja
na wilaya zake kuhusu ujio huu na kwamba kila mwandishi ajiandae na wazo lake
la habari la kiuchunguzi ambalo 'ataliuza' kwa magwiji wa TMF.
Msisitizo ni
kwamba wazo hilo liwe lenye kulenga kuleta uwajibikaji au mabadiliko katika
jamii husika.
Napenda ieleweke kwamba TMF itagharamikia malipo ya ukumbi, chai ya saa
nne, chakula cha mchana na chai ya saa kumi jioni. Hakuna malipo mengine yoyote
kwa waandishi.
Ni hayo tu kwa leo.
Au wasiliana na Gordon Kalulunga 0754 440749
kalulunga2006@gmail.com
Wasalaam,
Japhet
Sanga,
Communications/Individual Grants Officer
Tanzania Media Fund,
Dar Es Salaam.
+255 787 465 762
Communications/Individual Grants Officer
Tanzania Media Fund,
Dar Es Salaam.
+255 787 465 762
TMF Info
<info@tmf.or.tz>
Hivos
Tanzania/Tanzania Media Fund.
We have moved from 127 Mafinga Street,
We have moved from 127 Mafinga Street,
Kinondoni
to Kalenga/Uluguru Street, Plot 550A,
Upanga
Area (Near Muhimbili National Hospital Exit Gate).
0 comments:
Post a Comment