Monday, June 23, 2014

"MNATAKA KUNIULIA MAMA ANGU?" WEMA SEPETU AFUNGUKA KWA UCHUNGU BAADA YA WATU KUMTUKANA MAMA YAKE MZAZI

WEMA Sepetu ameonekana kufungukia wale wanaomtukana kila siku na sasa kufikia hatua ya kumtukana hadi mama yake mzazi...Kupita mtandao mmoja wa kijamii, Picha  moja  ya  mama  mzazi  wa  Wema  Sepetu  iliyotengenezwa  na  kuwa  CHAFU  ilitolewa  na  kisha  kuanza  kushushiwa  matusi  mazito...
 
Baada  ya  Picha  na  Matusi  hayo, Wema amefunguka kwa uchungu kwa kuandika: 
 "Dah...! Sijui hata niseme nini...! Ila si mlitaka kuniumiza... leo mmefanikiwa... nawapeni hongera.... Tena mmetisha haswa... Kila siku huwa hata siumizwi na matusi yenu cuz naonaga kama ni mnajisumbua tu… 
Hakuna siku nimelia kwa uchungu kama leo…
"I min mnitukane mimi mpaka mchoke but leave my mum out of it... Kawakosea nini nyinyi mama angu mpaka mfanye hivyo... Mzazi nwenyewe ndo nimebakia nae mmoja tu... mnataka afe na yeye nibaki yatima sio... dah... leo mmeniweza... saana jamani... Basi naomba isifike huko... nina uchungu sana na mama angu ... nampenda sana mama angu ila naona mnataka kuniulia mama angu… 
"Picha halisi ndo hio hapo juu kweli mtu uende ukamfanyie hivyo mama wa mwenzako... una mama wewe.. au uliokotwa na hujui uchungu wa mama... dah... nime surrender leo.... hongera zenu narudia tena... mmeniweza leo.... dah…
"Mungu nipe nguvu ktk hili jamani... Kwani nilichokikosea haswa ni kitu gani mpaka iwe hivi . Nimekosa nini mimi yarabi toba.... Eeeh mungu... Dah... Ila nashkuru..." Ameandika Wema  Sepetu  kwa Uchungu

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI