
Martha John katikati akiwa na washindi wa nafasi ya pili na ya tatu baada ya kutangazwa mshindi wa taji la Redds Miss Iringa 2014 jana katika ukumbi wa St Dominic huku mshindi wa pili ni Elizabeth Titus na mshindi wa tatu ni Foe Mkuchu.
(Picha na Francis Godwin)
…………………………………..
…………………………………..
Na Francis Godwin blog, Iringa
MREMBO Martha John kuuwakilisha mkoa wa Iringa katika mashindano ya Redds Miss kanda ya nyanda za juu kusini baada ya kufanikiwa kutwaa taji la Redds Miss Iringa 2014 baada ya kuwashinda washiriki wenzake nane waliojitosa katika kinyang’anyiro hicho .
Martha alitawazwa kuwa mrembo wa mkoa wa Iringa jana usiku katika ukumbi wa St Dominic shindano lililoshuhudia na kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa Gerald Guninita .
Kutokana na ushindi huo Martha kwa sasa ndie atakayeuwakilisha mkoa wa Iringa katika shindano la kumsaka Redds Miss Kanda ya nyanda za juu ,onyesho linalotarajia kufanyika ijumaa ya wiki ijayo mjini Iringa.
Jaji mkuu wa shindano hilo Dosi Magambo mbali ya kumtangaza Martha kuwa mshindi wa kwanza katika kinyang’anyiro hicho pia alimtangaza mshindi wa pili kuwa ni Elizabeth Titus na mshindi wa tatu ni Foe Mkuchu
Akikabidhi zawadi kwa washindi hao kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa Bw Guninita alisema kuwa ni imani yake na ya serikali ya Rais Dr Jakaya Kikwete kuona wasanii na washiriki wa michezo mbali mbali wanaendelea kufanya vema katika nafasi zao ili kuiwezesha nchi kupiga hatua katika sanaa mbali mbali.
0 comments:
Post a Comment