UGANDA
The Cranes imefanikiwa kusonga hatua inayofuata katika michuano ya
kuwania kupangwa hatua ya makundi kusaka tiketi ya kucheza fainali za
kombe la mataifa ya Afrika, AFCON 2015 nchini Morocco baada ya
kufanikiwa kuiondosha Madagascar kwa wastani wa mabao 2-2, lakini Uganda
wamenufaika kwa faida ya bao la ugenini.
Uganda
jioni hii wameibuka na ushindi wa bao 1-0 mjini Kampala katika mchezo wa
marudiano, na mechi ya kwanza walilala kwa mabao 2-1 nchini Madagascar.
Bao pekee
la Uganda limefungwa na Geoffrey Massa katika dakika ya 12 ya kipindi
cha kwanza na kuwasimamisha vitini mashabiki waliofurika kuitazama timu
yao.
Katika
mchezo mwingine uliomalizika jioni hii, timu ya taifa ya Rwanda
``Amavubi` imefanikiwa kusonga mbele kwa wastani wa mabao 3-0 kutokana
na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Libya walioupata jioni hii.
Mabao yote ya Rwanda yamefungwa na Dady Birori katika dakika ya 39`, 64 na 72.
Mechi ya kwanza Rwanda walitoka suluhu ya bila kufungana na Libya mjini Tripoli.
Mechi
nyingine zinazopigwa leo ni baina ya Guines Bissau dhidi ya Jamhuri ya
Afrika ya kati, wakati nao Sierra Leone watachuana na Swaziland.
Mechi baina ya Seychelles dhidi ya Gambia imeahirishwa.
0 comments:
Post a Comment