Wednesday, May 28, 2014

ANGALI SAFARI YA MWISHO YA MWANAHABARI MKONGWE MAXMILLIAN NGUBE ALIYEKUWA MPIGA PICHA WA MLIMANI TV!!!

Picha ya marehemu Max iliyopambwa kwa maua msibani, katika viwanjwa vya leaders hii leo.
Maximilian Ngube 'Max', enzi za uhai wake.
Max (kushoto), akiwa katika moja ya kazi zake enzi za uhai wake. Kulia ni Elizabeth Mramba walipokuwa wakitayarisha kipindi cha afya.
MPIGA PICHA mkongwe wa Televisheni, Maximilian Ngube 'Max' aliyefariki dunia siku ya Ijumaa Mei 23, 2014, jijijini Dar es salaam na hivi leo kuzikwa katika makaburi ya kinondoni.
 
Marehemu amewahi kufanyia kazi vituo kadhaa vya televisheni nchini, vikiwemo vya Star TV na Mlimani TV ambako ndiko alikuwa hadi kifo kinamkuta.
Ambapo hivi leo huzuni na simanzi vimetawala katika viwanja vya leaders Club, na wengi wao wakiukumbuka ucheshi, utani, mchango na umahiri wake katika Tasnia ya Habari.
Maximillian Ngube alizaliwa mwaka 1960 nchini Congo na baadae kuhamia nchini tanzania na kujiunga na timu ya mpira ya Yanga Sport club kabla ya kujiunga na tasnia ya habari.
Wanahabari wakiwa na majonzi baada ya kumuaga kipenzi wao Max



Rose ambaye ni mtoto wa marehemu Max, akilia kwa uchungu wakati wa kumuaga baba yake kipenzi marehemu Max

Watoto wa marehemu wakimuaga Papaa Max katika viwanja vya leaders hii leo na kuzikwa katika makabuli ya kinondoni. 
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU PEMA PEPONI 
AMEEN!

1 comments:

ZILIZOSOMWA ZAIDI