Wednesday, April 9, 2014

FT: YANGA SC 2 VS 1 KAGERA SUGAR UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM

FT: YANGA SC 2 VS 1 KAGERA SUGAR
Hussein Javu anapiga shuti kali lakini kipa Agaton Antony anaokoa
Dakika 45 kwa mujibu wa saa yetu zimeshakimilika

Dakika ya 40` Yanga bado wanaongoza kwa mabao 2-1

Dakika ya 37` Kagera Sugar wanaonesha upinzani mkubwa, lakini Yanga wanapoteza nafasi nyingi za kufunga

Dakika a 36` kipindi cha pili Nizar Khalfan anapasha moto misuli yake, bila shaka anataka kuchukua nafasi ya mtu

Dakika ya 25` kipindi cha pili, timu zote zinashambuliana kwa zamu.

Dakika ya 21` ya kipindi cha pili, Kagera Sugar wamechangamka zaidi baada ya kupata bao.

Dakika ya 19` Mrisho Khalfan Ngasa anakwenda benchi, nafasi yake inachukuliwa na Hussein Javu

Dakika ya 18` kipindi cha pili, Daudi Jumanne anaisawazishia Kagera Sugar bao la kwanza kufuatia beki wa pembeni, Oscar Joshua kuzembea kuosha mpira.

Dakika 11` kipindi cha pili zimeshaondoka, Yanga wapo mbele kwa mabao mawili kwa bila.

Hussein Javu aliyeko katika kiwango kizuri sasa anapiga jalamba.

Dakika ya 7` kipindi cha pili, Mbuyu Twite anaoneshwa kadi ya njano na mpira ni faulo kuelekea lango la Yanga

Dakika ya 7` Hamis Kiiza almanusura aandike bao la tatu kwa Yanga.

Dakika ya 6` kipindi cha pili, Mrisho Ngasa anaachia shuti kali linatoka sentimita chache kwenye lango la Kagera.

Kipindi cha pili, Mpira umeshaanza hapa uwanja wa Taifa.

Yanga wanaingia uwanjani wakiongozwa na Didier Kavumbagau.

Kipindi cha pili karibu kinaanza, wachezaji wa Kagera Sugar wameshaingia uwanjani na wa Yanga bado.
............................................

Kwa ujumla Yanga walicheza vizuri ndani ya dakika 30 za kwanza, lakini dakika 15 za mwisho ndani ya kipindi hicho, cha kwanza, Kagera Suagr walikuwa na makali zaidi na isingekuwa umahiri wa kipa Dida wangepata bao


HT: YANGA SC 2 VS 0 KAGERA SUGAR

Dakika 45 kipindi cha kwanza Daudi Jumanne alipiga shuti ambalo lilikuwa hatari, lakini Dida ameokoa 

Dakika 41` kipindi cha kwanza Yanga wanaongoza kwa mabao 2-0.

Dakika ya 37` bado Yanga wanaongoza kwa mabao 2-0

Dakika 34` kipindi cha kwanza Didier Kavumbagu anaipatia Yanga bao la Pili. 

Dakika ya 31` kipindi cha kwanza bado Yanga wanaongoza kwa bao 1-0

Dakika ya 15` Yanga 1 kagera sugar sifuri.

Dakika ya 7` kipindi cha kwanza Yanga bado wanaongoza kwa bao 1-0

Dakika ya 3` kipindi cha kwanza Hamis Kiiza `Diego` anaipatia Yanga bao la kwanza akimalizia krosi ya Mrisho Ngasa

Mpira umeshaanza hapa uwanja wa Taifa

Mpira unaanza muda wowote kutoka sasa.

Manahodha wa timu zote wanaitwa kuchagua milango ya kuanza

Wachezaji wameshaingia uwanjani na wanapiga picha za kumbukumbu.

Wachezaji wanaoanza wapo kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, wachezaji wa akiba wameshakaa katika mabenchi yao

YANGA SC 2 VS 1 KAGERA SUGAR.......................................................................................................................
Here's Young Africans line-up to face Kagera Sugar today:
1. Deo Munish "Dida" - 30
2. Juma Abdul - 12
3. Oscar Joshua - 4
4. Nadir Haroub "Cannavaro" - 23
5. Mbuyu Twite - 6
6. Frank Domayo - 18
7. Saimon Msuva - 27
8. Hassan Dilunga - 26
9. Didier Kavumbagu - 7
10. Mrisho Ngasa - 17
11. Hamisi Kizza - 20

Subs:
1. Barthez, 2. Job, 3. Telela, 4. Zahir, 5. Nizar, 6. Javu, 7. Jerson Tegete

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI