Wednesday, April 30, 2014

DIDIER KAVUMBAGU AIPA KISOGO YANGA, ASAINI AZAM FC



Na Mwandishi Wetu, Dar
MSHAMBULIAJI na mpachika mabao wa Yanga na Nahodha wa timu ya Taifa ya Burundi, Didier Kavumbangu, leo mchana amesaini Mkataba wa miaka miwili na mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam FC.
Kavumbangu aliyemaliza Mkataba wake wa miaka miwili Yanga SC, ameamua kusaini Azam FC baada ya kuona Klabu yake haina mawasiliano naye licha ya kumaliza Mkataba wake.
“Mimi ni mchezaji, kazi yangu ni mpira. Nimemaliza mkataba Yanga, lakini viongozi hawaniambii kitu, nimepata ofa nzuri Azam nikaamua kusaini,” amesema
Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi, Kavumbangu, baada ya kusaini Mkataba huo ambao unamfanya alipwe vizuri kuliko alivyokuwa analipwa Jangwani.

Pamoja na hayo, Kavumbangu ameishukuru Yanga SC na mashabiki kwa miaka miwili aliyoichezea timu hiyo na anasema itabakia kwenye kumbukumbu zake kwa kushinda nayo mataji kadhaa.
Mshambuliaji huyo mrefu mwenye nguvu amesema sasa akili yake anaipeleka kwa mwajiri wake mpya, Azam FC ambako pia amepania kwenda kushinda mataji na kuiwezesha timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika.  
“Mimi sasa ni mchezaji wa Azam, nafurahi kujiunga na klabu hii kubwa. Kawaida yangu huwa nashabikia klabu nayochezea, sasa mimi ni mshabiki namba moja wa Azam,”amesema.   

Kavumbangu alitua Yanga mwaka 2012 akitokea Atletico ya Burundi na katika mechi misimu miwili ya kuichezea klabu hiyo, amefunga mabao 31 katika mechi 63 za mashindano yote, moja tu la penalti.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI