Saturday, March 1, 2014

NDOA YA MSANII ROBIN THICKE NA MKEWE PAULA YAVUNJIKA

SUALA la kutodumu katika ndoa kwa wasanii wakubwa duniani hasa wasanii wa muziki, si jambo la kushangaza sana, kwani wengi wao huishi miaka michache na kuamua kila mmoja kushika hamsini zake.

Na inapotokea wawili hao wakadumu basi ndoa zao huwa na mshike mshike kitu ambacho mara nyingi hupelekea mpalaganyiko katika ndoa siku za baadae.

Hivi karibuni mwanamuziki maarufu duniani wa muziki wa RnB na Hip Hop, Robin Thicke ambaye alimuoa mwigizaji maarufu Paula Patton aliye igiza katika filamu ya About last night, walitengana rasmi na mwanamama huyo licha ya kuishi pamoja katika maisha ya ndoa kwa miaka kumi.
Robin na Paula
Miezi ya hivi karibuni taarifa zao zimekua zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii na vituo mbalimbali vya radio na televisheni juu ya misuguano iliyopo katika ndoa yao.
Taarifa ya kutengana kwa wasanii hao maarufu imetolewa rasmi na mkewe Paula Paton, ambapo baadae wanandoa hao walisisitiza kua siku zote wataendelea kupendana na kuwa marafiki wa karibu, na suala la kutengana kwao ni jambo ambalo wameliamua kwa pamoja hivyo hakuna wakulaumiwa.

Robin Thickle mwenye umaarufu duniani tangu miaka ya tisini, alikutana na mkewe akiwa na umri wa miaka 14 katika ukumbi mmoja wa burudani na akamuomba wacheze wote nyimbo ndipo akamuimbia nyimbo ya Stevie Wonder ya Jungle Fever, baadae urafiki wao kaanza huku yeye (Robin) akiwa na umri wa miaka 16 na mnamo mwaka 2005 Robin na Paula waliamua kuyachukua mahusiano yao katika ngazi ya juu zaidi kwa kuamua kufunga ndoa.
Paula Paton
Wawili hao wamebarikiwa mtoto mmoja wa kiume Julia fuego aliyezaliwa mwaka 2010.
Robin na Paula wakiwa na mtoto wakifurahia maisha ufukweni.

Kwa sasa Robin ni mwimbaji maarufu anayetamba na kibao chake kiitwacho Blurred lines alichomshirikisha mwanamuziki T.I na Pharrell ambapo kibao hicho ndicho kilichobeba albam yake ya sita ambayo inaitwa Blurred lines. na amefanya vibao vingine vingi kama 'Lost Without you', 'It's In The Morning alichomshirikisha Snoop Dogg.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI