Msuluhishi wa kisheria wa sakata la madai ya klabu ya Simba dhidi ya Yanga kwenye usajili wa mchezaji Hassan Kessy, Mzee Said El-Maamry apanga kukutana na pande zote Alhamisi ya Novemba 3, mwaka huu.
Awali msuluhushi huyo alishindwa kuendelea na kikao hicho baada ya taarifa kutoka kwa Yanga ikidai kuwa mmoja wa wawakilishi wake, wakili Alex Mgongolwa alifiwa hivyo kuomba kupangiwa siku nyingine.
“Ili kutenda haki, lazima tutoe nafasi kwa pande zote kusikiliszwa. Ni vema Mwanasheria wa Young Africans akasubiriwa,” amesema msuluhishi huyo.
Kutokana na hali hiyo mzee El-Maamry amepanga sasa kukutana na viongozi na wawakilishi wa pande zote mbili kwenye ofisi za TFF ili kuangalia namna ya kumaliza madai hayo ya Simba likiwemo la kuwashtaki Yanga na jingine ni dhidi ya mchezaji mwenyewe [Hassan Kessy].
Kamati ya TFF iliyoteuliwa hapo awali kusikiliza shauri hilo inasubiri makubaliano hayo ili kama ikitokea imeshindikana, suala hilo litarudi kwenye kamati hiyo kwa ajili ya uamuzi wa mwisho kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sheria zinazoongoza mpira wa miguu.
0 comments:
Post a Comment