Wiki hii nchi ya China imefanikiwa kurusha roketi yake kubwa zaidi ambayo haijawahi kurushwa ndani ya taifa hilo.
Roketi hiyo imepewa jina la Long March 5 ilirushwa angani kutoka kituo cha anga za juu cha Wenchang huko Hainan huku ikiwa imebeba setilaiti ya kufanyia majaribio inayojulikana kama Shijian-17.
Imedaiwa kuwa Long March 5 inauwezo wa kubeba vitu ikiwemo mitambo yenye uzito hadi kufikia tani 25 hadi chini ya dunia huku ikikadiriwa kubeba tani 14 ya mzigo hadi kufikia umbali wa kilometa 36,000 kutoka umbali wa dunia.
Mwezi uliopita China ilipeleka angani chombo chake cha Shenzhou-11 kilichokuwa na wanajimu wawili ambacho kilipaa angani kutokea Jiuquan Satellite Launch Centre kwenye jangwa la Gobi.
Wakati huo huo shirika la anga za juu la Marekani (NASA) limepanga kuanza kufanya safari ya kwanza kwa roketi yake kubwa zaidi kuwahi kutokea ambayo inadaiwa kuwa na uwezo wa kubeba tani 130 huku ikitarajiwa kuanza safari yake ya kwanza kwenye sayari ya Mars mwaka 2018.
0 comments:
Post a Comment