Monday, November 16, 2015

SILAHA KIBWENE,MTU 23 MBARONI KWA UGAIDI UFARANSA

IDADI kubwa ya silaha imekamatwa katika msako unaoendelea kuwakamata waliohusika na mashambulio ya kigaidi mjini Paris , Ufaransa yaliyofanyika Ijumaa iliyopita.
Katika msako huo mkali watu 23 wameshatiwa mbaroni kusaidia polisi katika msako wao mkali wa kundi la magaidi lililotoka katika dola la Kiislamu.
Pamoja na msako huo kufanyika nchini Ufaransa, polisi wa Ubelgiji nao wameendesha msako mkali.
Katika mashambulio ya Ijumaa kwenye baa, mgahawa, nje ya uwanja wa mpira na katika jingo la kufanyia tamasha watu 129 waliuawa.
Wakati huo kaka  wa magaidi wawili  aliyekamatwa nchini Ubelgiji ameachiwa huru. Mwanasheria wa Mohammed Abdeslam alisema kwamba ameachiwa bila sharti lolote.
Kaka huyo ni ndugu wa Brahim Abdeslam, aliyeuawa katika shambulio hilo na mwingine Salah Abdeslam ambaye anatafutwa.
Watu saba walikamatwa nchini Ubelgiji mwishoni mwa wiki na Mohammed Abdeslam ni mmoja wa watu watano ambao waliachiwa huru.
Ufaransa leo ilisimama kimya kwa dakika moja kuwakumbuka wote waliouawa katika kadhia hiyo mbaya katika historia ya wakati wa amani nchini humo

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI