Monday, October 5, 2015

NINI MAONI YAKO JUU YA KAULI HII YA RAY KUHUSU YEYE KUIKIMBIA TEAM MABADILIKO?

Huku vuguvuga la uchaguzi likiendelea, leo mwigizaji maarufu nchini Vicenti Kigosi aliyekuwa anaongoza mapambano ya mabadiliko ndani ya UKAWA kabla ya kuhamia CCM ameandika ujumbe ufuatao kwa mashabiki wake..

“..Kwanza kabisa ningependa kuwaambia wafuata mkumbo mpende kupanua akili zenu na si kupenda kupanua vidole 2.

Nashangazwa sana na wapinzani kusimama mbele ya adhara na kusema kuwa tangia tumepata uhuru miaka 50 iliyopita serikali haijafanya chochote na wewe unashangalia tena anayekwambia hivyo ni kiongozi aliyekaa madaraka ni miaka 10 mwingine miaka miwili alafu sasa hivi hao hao ndio wanakwambieni kuwa watawaletea mabadiliko s'tukeni watanzania watatuingiza mkenge hawa wapinzani.

Ninaamini watanzania wanataka kupata m badala wa ccm kwa kipindi kirefu lkn mm naona bado kuwepo mbadala wa ccm maana hao ndio walewale waliotoka ccm. pateni uzoefu kwanza kwa sasa bado mtatupeleka gizani.


Baadhi ya watu wanasema kuwa wasanii wanaowasapoti ccm hawatonunua kazi zao wanamuziki wakiomba wapigiwe kura eti waambieni ccm wawapigie kura wanasahau kwamba msanii naye ana haki ya kuwa upande wa chama anayeutaka yeye kuna mifano mingi marekani wasanii walimsapoti obama nigeria wasanii walimsapoti muhammadu buhari.sio sisi wakwanza kufanya hivyo…”  Ray kigosi

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI