Sunday, October 4, 2015

KUNDEMBA YAANZA VYEMA LIGI DARAJA LA PILI YAIFUNGA RASCAZONE 3-2

Timu ya Kundemba FC leo imeanza mechi yake ya kwanza kwa ushindi wa magoli 3-2 katika ligi ya Daraja la Pili.

Kundemba ilicheza na timu ya Ras Cazone katika uwanja wa Amaan ambao ulianza saa 8:00 mchana.

Magoli ya Kundemba yalifungwa na Sadi Mgeni ambae kwa leo alikua captain yeye aweka kimiani magoli 2 yote kwa njia ya penalti.

Goli la 3 lilifungwa na Ali Abdalla almaarufu 'dume' mnamo dakika za 85 ambaye alitokea bench.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI