RAIS wa klabu ya AC Milan ya Italia Silvio Berlusconi
ambaye awali alikubali kuwa katika mipango ya kujenga uwanja mpya wa
klabu hiyo na kuachana na mpango wa kuendelea kutumia uwanja wa San Siro.
Stori zilizoingia katika headlines hivi karibuni ni kuwa amesitisha
mpango wa kujenga uwanja mpya wa klabu hiyo kwani bado wanamapenzi na San Siro.

Awali kulikuwa na stori za klabu hiyo kupewa zawadi ya kujenga uwanja wa klabu yao kati kati ya mji wa Lombardy, mji ambao unatajwa kuwa na idadi ya watu milioni 10. Binti wa Silvio Berlusconi, Barbara alikuwa akiongoza mipango ya ujenzi wa uwanja ambao ungeanza 2018-2019.
San Siro
Uwanja huo ambao ungekuwa na uwezo wa
kuchukua watu 48000, umtengazwa kusitishwa kwasababu alizozitaja kuwa
bado klabu yake ina furaha kutumia uwanja wa San Siro. Klabu za AC Milan na Inter Milan zote hutumia uwanja wa San Siro kama uwanja wao wa nyumbani ila ukitumiwa na klabu ya Inter Milan kama uwanja wa nyumbani unaitwa jina la Giuseppe Meazza.
0 comments:
Post a Comment