MAMBO 5 YANAYONIPA AMANI YA KUWAWAPA DHAMANA UKAWA FOR 2015-2020
i. Elimu
ii. Katiba mpya
iii. Usimamizi wa utawala wa sheria na uwajibikaji
iv. Ulinzi wa rasilimali hasa gesi na mafuta
v. Chachu ya vijana/ushirikishaji wa vijana
vi. Dhana ya mabadiliko/changes:
A. Elimu, Elimu, Elimu
Tushabikie kitu chenye uhalisia kwa fahari bila kuogopa, tusiwakosoe kuwa serikali yao itawezaje kuitekeleza sera hii muhimu, bali tutafakari umuhimu wake ili tuone namna ya ku support iweze kutimia
Mataifa mengi yamepata mapinduzi makubwa kiuchumi kupitia elimu, mfano UK and US elimu yao ni bure bure bure na ni elimu bora, wata compromise kwenye maeneo mengine but they dont mess up with education....kama unaona mbali utakubaliana na mimi kuwa hata Jamhiri ya Uchina, Malasia, Singapore, South Korea, Japan ni Elimu kwa vijana wao iliwekwa kuwa kipaumbele na hapo vijana hawa wakaja kuikoa nchi
2014 Marekeni walitumia $3.5trilion kwenye education ambayo ni sawa na 20% ya budget katika mwaka wa fedha
Faida za elimu
1. Huondoa ujinga
2. Huongeza ujaziri, confidence
3.Hujenga ubunifu
4.Huimarisha ushindani.
Elimu tunayoitaka:
1.Free education: Elimu bora/quality, waalimu bora, mazingira bora maslahi....tangu elimu ya awali mpaka university, tufike mahali mtu akitaka kumsomesha mwanae private schools iwe ni hiari tu ila siyo kwa sababu elimu ya Umma siyo BORA
2. COMPETITIVE EDUCATION KWA HIGHER LEARNING: ELIMU YENYE UBORA NA USHINDANI
3. Capacity and infrastuctures za kutosha ili watu wote wanaotaka kusoma wapate nafasi.
4.Maarifa ya kazi/home craft iwe ni sehemu ya lazima katika elimu
5.National service ni compusory kwa wahitimu wa form six
6.Uwekezaji katika sayansi na technology upewe kupaumbele
7. Kusomesha vijana wetu vyuo vya nje kwa wingi pale inapokuwa hakuna nyenzo hizo hapa nyumbani
8.Tafiti endelevu/vyuo vya tafiti nk
B. KATIBA MPYA:
KATIBA YA WANANCHI ITEKELEZWE KWA DHATI: RASIMU YA WARIOBA
C. RASILIMALI/GAS + MAFUTA:
1.sera nzuri ya uwekezaji, wizara pekee ya kushughulikia eneo hili
2. Ulinzi wa rasilimali zetu.
D. UTAWALA WA KISHERIA:
Sheria nzuri isiyokandamiza na inayofuatwa:
E. CHACHU YA VIJANA:
Sehemu nyingi duniani ukiona vijana wanaingia kwenye jambo ujue mapinduzi ya kweli yanaendakutokea, hili ni jambo liko hivyo kihistoria.
Inasemekana asilimia kubwa ya wapiga kura wa mwaka huu ni vijana, hili ni jambo la heri pia kwa kuwa zaidi ya 60% ya Tz ni vijana, hivyo
wakiamua wanaamua sawasawa na matakwa yanayowahusu zaidi. Jambo hili linatiwa chachu na ukweli kwamba hata wagombea waliowengi ni vijana.
F. DHANA YA MABADILIKO:
Changes are inevitable: Falsafa ya mabadiliko ilimpa OBAMA ushindi mwaka 2008: ni dhana kubwa yenye maana kubwa pia:
"Big changes in your life may be to move to a new city, state, or country, or a change in jobs. You can even try really hard to change who runs the government. In fact, that last type of change is probably one of the biggest a group of people can experience. When there is a significant disruption in a government that leads to new or modified leadership or policies, we call this type of change political change"
Kimsingi tuache ushabiki, tuhurumie vizazi vijavyo, Nigeria waliona hilo na kuamua kwa pamoja hata wanachama wa PDP wakamnyima kura rais G. Jonathan na Kumchagua Gen. Muhammadu Buhari wa APC kwa 53.96% Huku chama tawala wakiabulia 44.96% ya kura zote:
Nguvu ya umma hutumika kwa maslahi ya umma, kuziondoa tofauti zetu za kivyama na kuamua kubadilisha serikali, bila kujali upo chama gani..mambo kama haya hufanyika hata Marekani...bila kujali uchama watu huamua kupiga kura kiuzalendo zaidi
KARIBU TZ MPYA YA UKAWA:
MUNGU IBARIKI TZ
0 comments:
Post a Comment