Tuesday, September 1, 2015

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS ZANZIBAR, MAALIM SEIF AKAGUA UWANJA WA NDEGE NA BANDARI YA MALINDI ZANZIBAR


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Zanzibar Bw. Said Ndubugani, akimueleza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, juu ya hatua zinazochukuliwa na mamlaka hiyo katika kuimarisha viwanja vya ndege, alipofanya ziara ya kutembelea eneo hilo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akitembelea maeneo mbali mbali ya uwanja wa ndege wa Zanzibar katika ziara yake ya kutembelea eneo hilo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiangalia maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Zanzibar alipotembelea eneo hilo.
Mratibu wa ujenzi wa jengo jipya la abiria (terminal 2) katika uwanja wa ndege wa Zanzibar Bw. Yasser De Costa akimueleza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, juu ya maendeleo ya ujenzi huo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiangalia maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Zanzibar alipotembelea eneo hilo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Maalim Seif Sharif Hamad, akiangalia baadhi ya bidhaa zinazopatikana ndani ya duka la uwanja wa ndege wa Zanzibar, na kutoa wito wa kuzitangaza bidhaa zinazozalishwa hapa nchini zikiwemo karafuu na vitu vya sanaa.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiangalia baadhi ya bidhaa zinazopatikana ndani ya duka la uwanja wa ndege wa Zanzibar, na kutoa wito wa kuzitangaza bidhaa zinazozalishwa hapa nchini zikiwemo karafuu na vitu vya sanaa.
Raia wa Syria Bw. Mark Bachayani (kushoto) akijinasibu kupiga picha na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika ziara ya kutembelea uwanja wa ndege wa Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Bw. Abdallah Juma, akimueleza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, juu ya hatua zinazochukuliwa na shirika hilo katika kuimarisha huduma wakati wa ziara yake ya kutembelea eneo hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Bw. Abdallah Juma, akimueleza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, juu ya hatua zinazochukuliwa na shirika hilo katika kuimarisha huduma wakati wa ziara yake ya kutembelea eneo hilo
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na watendaji wa Shirika la Bandari Zanzibar, wakati akihitimisha ziara yake ya kutembelea eneo hilo
(Picha na Salmin Said, OMKR)
Na: Khamis Haji (OMKR)
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amewahimiza viongozi wa Bandari na viwanja vya ndege Zanzibar kuzidisha bidii katika utendaji wao na wahakikishe usalama wa wananchi na wageni wanaotumia maeneo hayo ni wa uhakika.

Maalim Seif amesema hayo leo wakati alipotembelea uwanja wa ndege wa Zanzibar na Bandari ya Malindi kufuatilia utekelezaji wa majukumu mbali mbali katika maeneo hayo, ikiwemo miradi inayoendelea kutekelezwa.

Katika uwanja wa ndege wa Zanzibar, Makamu wa Kwanza wa Rais alipongeza juhudi kubwa zinazochukuliwa kukamilisha ujenzi wa jengo jipya la abiria (Terminal 2)
Maalim Seif amesema mashirika mengi ya ndege ya Kimataifa yameonesha nia ya kuleta ndege zao Zanzibar, hivyo hatua ya kuwa na uwanja wa ndege wa kisasa wenye hadhi ya Kimataifa, kama ambavyo litakuwa jengo hilo litakapokamilika na kuanza kutoa huduma, itaiwezesha Zanzibar kukuza mapato yake na kujipatia sifa kubwa kitaifa na kimataifa.
Mratibu wa ujenzi wa jengo hilo, Yassir De Costa amesema jengo jipya litakapokamilika litakuwa na huduma zote zinazohitajika kwa uwanja wa ndege wa Kimataifa na litaweza kuhudumia abiria wanaosafiri ndani na wale wanaoingia na kutoka nje ya nchi.

Aidha, Maalim Seif amewahimiza viongozi wa Mamlaka ya Anga Zanzibar kuchukua hatua maalum kuhakikisha Zanzibar inakuwa na wataalamu wengi katika masuala ya usafiri wa anga, ili kukabiliana na uhaba wa wataalamu hao uliopo hivi sasa.

Akiwa katika bandari ya Malindi, Makamu wa Kwanza wa Rais alipongeza hatua nzuri iliyochukuliwa na Shirika la Bandari kuhakikisha inapunguza msongamano wa makontena uliokuwepo na kusababisha usumbufu mkubwa, ikiwemo ukosefu wa nafasi ya kuweka mizigo inayoingia.

Amesema miongoni mwa hatua zinazopaswa kuchukuliwa na Shirika la Bandari ni kujijengea uwezo wa mawasiliano kati yake na vyombo vyote vinavyo safari baharini, ili kuweza kubaini kwa haraka pale ajali zinapotokea, na kuhakikisha sheria zinafuatwa na vyombo vyote vya usafiri wa baharini.

Ameeleza kuwa Bandari ni eneo muhimu ambalo linahitajika liwe na utaratibu mzuri unaoeleweka wa ulinzi na usalama, na ni jambo la lazima kwa abiria na watumiaji wote wa eneo hilo wanafuata taratibu za usalama zilizowekwa kwa faida yao na taifa kwa ujumla.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar, Abdallah Juma amesema suala la ulinzi na usalama limepewa umuhimu wa kipekee katika eneo lote la Bandari hiyo kazi ambayo wanaifanya kikamilifu kwa ushirikiano na vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo katika eneo hilo. Katika ziara hiyo ya siku moja, Maalim Seif alifuatana na Naibu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano, Mhe. Issa Haji Ussi na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Juma Malik Akili.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI