MGOMBEA Ubunge wa jimbo la Iringa Mjini kupitia ACT Wazalendo Bi Chiku Abwao(pichani) amesema heri ya miaka mitano ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Mobica Mbega ( CCM) kuliko miaka mitano ya Mchungaji Peter Msigwa ( Chadema)hivyo ametawa mwaka huu wananchi kumchagua yeye
Akizungumza katika mkutano wake wa kampeni za Ubunge jana kata ya Kihesa alisema iwapo atakuwa mbunge wao atahakikisha anakuwa mbunge wa mfano wa kuwaletea maendeleo sahihi.
Kwani alisema kuwa historia ya jimbo hilo mwaka 1995 walichagua NCCR mageuzi ambapo Bw Mfalamagoha Kibasa kuwa mbunge ila baada ya kushindwa kutekeleza ahadi zake mwaka 2000 walimchagua Monica Mbega ( CCM) ambae kipindi cha kwanza alifanya Kazi vizuri na mwaka 2005 wananchi walimchagua tena ila hakuweza kufanya Kazi ndipo walipomchagua Mchungaji Peter Msigwa( Chadema) ambae hajafanya Kazi yoyote.
Hivyo alisema kwa sasa imani yake juu ya wanaume kuwa wabunge katika jimbo hilo haipo tena kwani hawana nia ya kweli ya kuwatumikia wananchi na kudai kuwa iwapo mbunge aliyemaliza muda wake mchungaji Msigwa angetekeleza ahadi zake vema leo asingesimama kugombea ubunge bali angemuunga mkono mbunge huyo ili aendelee kwa kipindi cha pili ila kwa kuwa hakuna jipya alilolifanya hana imani nae na hivyo ni wakati wa wananchi wa jimbo hilo kuwapima wagombea wengine waliojitokeza nje ya mbunge huyo .
Alisema ahadi za mbunge aliyemaliza muda wake zilikuwa zaidi ya 14 ikiwemo ya kuwawezesha wananchi waliojiunga katika vikundi kupatiwa mitaji ya kuanzisha biashara kwa wakati huo alisema yeye si mbunge wa kutoa pesa bali atawawezesha kiuchumi kwa kuwapa nyavu (mitaji) ila baada ya kuwa mbunge alianza kuwasema vibaya wananchi kwa kudai yeye si mbunge wa kutoa pesa (ATM)pia aliahidi ujenzi wa soko la kisasa Kihesa na kumweka mwanasheria katika ofisi yake ila hadi sasa hakuna alichofanya na akikumbushwa hukimbilia kujenga chuki na kila mtu .
Bi Abwao ambae amepata kuwa mjumbe wa kamati kuu ya Chadema Taifa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia Chadema alisema kuwa hali ya chadema na UKAWA kwa sasa imepoteza mwelekeo na chadema kugeuka ni chama cha kutetea mafisadi tofauti na iliyokuwa awali kuwa chama cha kupinga ufisadi .
Hivyo alisema sababu ya kukihama chama hicho na kujiunga na ACT wazalendo ni kutafuta chama cha upinzani makini ambacho atawatumikia wananchi bila ya kuwajengea maswali kama ilivyo hivi sasa kwa mgombea wa Chadema Iringa mjini mhungaji Msigwa ambae alikuwa mbele kupinga ufisadi na hata kusema wanaomuunga mkono aliyekuwa waziri mkuu Edward Lowassa ambae ni mgombea wa Chadema kwa sasa wakapimwe akili zao .
Alisema Chadema kwa sasa imekuwa ni chama cha kupiga dili akiwemo aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Mchungaji Msigwa ambae leo kati ya maswali magumu ambayo anahojiwa na wapiga kura wake ni juu ya kauli yake dhidi ya wale wanaomuunga mkono LOwasa kutakiwa kupimwa akili zao.
Akielezea kuhusu sera zake kwa wananchi wa jimbo la Iringa mjini iwapo watamchagua kuwa mbunge wa jimbo hilo atahakikisha anautumia vema mfuko wa jimbo kwa kuwasaidia wazee ,vijana na wanawake kuwa na vikundi vya kiuchumi tofauti na ilivyokuwa awali miaka mitano iliyopita kwa mfuko huo kushindwa kufanya kazi yoyote.
Pia kuhakikisha anaibana serikali ili vijana kupewa mikopo nafuu na kuzuia posho kwa watumishi wa umma ambazo zimekuwa zikikwamisha maendeleo katika jimbo hilo .
0 comments:
Post a Comment