KIWANGO! Tofauti
na watu wengine ambao maumbile yao hubadilika mara baada ya kujifungua,
kwa staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel hali imekuwa tofauti, uzuri
na umbo lake limebaki vilevile.
Akizungumza na wahariri sambamba na waandishi wa Global Publishers
nyumbani kwake Mwananyamala jijini Dar, Aunt alisema kilichomfanya
asinenepe kupita kiasi na kuharibika mwili ni mazoezi sambamba na
kufuata ushauri wa vyakula anaopewa hivyo mwili wake kubaki vilevile.
“Nachukia ubonge nyanya, namshukuru Mungu pia kwani wengi wakijifungua
huwa wananenepa hovyo lakini kwangu mambo yamekuwa tofauti. Niko
vilevile, nafikiri pia ni kutokana na kufuata ushauri mzuri wa kula
chakula niliopewa,” alisema Aunt.
Mbali na kutobadilika, Aunt alisema kwa sasa muda mwingi anautumia kuwa
nyumbani na ubavu wake, Moze Iyobo wakimlea mtoto wao tofauti na zamani
alipokuwa na misele ya usiku katika viwanja tofauti vya starehe.
0 comments:
Post a Comment