Friday, May 1, 2015

MKE AANDAA FUMANIZI USIKU WA SAA 5 MOROGORO, KILICHOTOKEA MMH..!

Akiwa na shoga yake.
Dustan Shekidele, Morogoro
MWANAMKE mmoja aliyefahamika kwa jina la Janeth, hivi karibuni alizua kizaazaa cha aina yake baada ya kumtegea mumewe fumanizi kufuatia madai kuwa anachepuka lakini likadunda.Tukio hilo lilitokea mwanzoni mwa wiki hii, saa 5 usiku katika Mtaa wa Bigwa, Kata ya Kilakala mkoani Morogoro.
Janeth anayedaiwa kumtegea mumewe fumanizi. Chanzo chetu cha kuaminika kilidai kuwa, siku ya tukio Janeth alitonywa na wambeya kuwa mumewe eti yuko nyumbani kwa mwanamke mmoja ambaye ni mama n’tilie (jina halikufahamika mara moja) na ndipo alipochukua wapambe wake na kwenda kumfumania.
“Siku hiyo mimi nilikuwa nyumbani kwangu, mara Janeth akanifuata na kuniambia kuwa nimpe kampani eti akamfumanie mumewe na mwizi wake.“Kwa kuwa nimeshibana naye, tukaongozana hadi eneo la tukio lakini tulichotaka kukifanya kilishindikana kwani tulikuta wamejifungia, tukagonga mlango ndipo mwenyekiti wa mtaa huo akafika na kuomba tuache kuwasumbua.
“Wakati sisi tukiwa nje tukisubiri watoke, tukaambiwa kuwa mwanaume tayari alitoroshwa kupitia mlango wa nyuma na kutimka. Tukafanya vurugu, watu wakajaa lakini kiukweli tuliumia sana kutomnasa,” alisema mmoja wa marafiki wa karibu wa Janeth. Akizungumzia tukio hilo, Janeth alisema: “Ana bahati yake, leo ningemnasa angenitambua, amshukuru huyo aliyemtorosha.”
#GP

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI