<3 <3 <3 WADADA NA WAKAKA INAWAHUSU<3 <3 <3
HIZI NI ISHARA 10 ZA MWANAUME ASIYEKUWA NA
MIPANGO NA WEWE..
1.HAPIGI SIMU, BALI HUTUMIA SMS
Je, Kijana Huyu Aliyekwambia Anakupenda Huwa Anawasiliana Nawe Kwa Njia
Ya Ujumbe Mfupi Kuliko Anavyokupigia? Kama Utaona Hivyo, Basi Una Kila
Sababu Ya Kuanza Kuitilia Shaka Nia Ya Kijana Huyu Wa kike/Kiume, Kwani Kwa
Hakika Hana Nia Yoyote Ya Dhati Ya Kuendelea Kuwa Nawe.
Kijana Wa Kiume/kike Anapompenda Msichana/mvulana, Hutamani Muda Wote Kuisikia Sauti
Yake. Anapokuwa Anasisitiza Kutumika Kwa Ujumbe Mfupi Maana Yake Hana
Haja Sana Ya Kusikia Sauti Yako.
Naam, Ujumbe Mfupi Wa Maneno Si Njia
Rahisi Sana Ya Kuwasiliana, Lakini Zaidi Ni Njia Rahisi Zaidi Ya Kuepuka
Mawasiliano Na Kutoa Majibu Mafupi Kwa Mtu Ambaye Usingependa
Kuwasiliana Naye.
2.HANA SABABU ZA KUCHELEWA
Unaweza Kubaini Katika Mikutano Yako Miwili-Mitatu Na Kijana
Aliyekwambia Anakupenda, Kwamba Si Mtu Wa Kujali Wala Kutunza Muda.
Naam, Yawezekana Katika Mara Mnazokutana, Mara Nyingi Zaidi Anachelewa
Kuliko Anavyowahi. Unaweza Kudhani Kuwa Kijana Huyu Ana Mambo Mengi, Au
Si Mzuri Katika Upangiliaji Wake Wa Muda, Lakini Kwa Hakika Hupaswi
Kumtafutia Visingizio Hata Kama Unampenda, Kwani Kuna Uwezekano Mkubwa
Kuwa Kijana Huyu Hana Mpango Na Wewe.
Kijana Wa Kiume/kike Akikupenda Na Kupenda Kuendelea Kuwa Nawe, Lazima Tu
Atakuwa Na Msukumo Wa Kutaka Kukutana Na Wewe Na Hatapenda Kukuudhi Kwa
Kuchelewa.
Mtu Huyu Hata Kama Atakuwa Amebanwa Vipi Kazini Ni Rahisi
Sana Kutafuta Muda Wa Kukutana Na Wewe. Kinyume Chake Atakuwa Ni Mtu Wa
Visingizio Vya Kuchelewa Na Wakati Mwingine Kutofika Kabisa Katika Eneo
La Miadi – Hususan Kama Ameshakupata.
3.ANAWASILIANA NA MPENZI WA ZAMANI
Mwanaume/Mwanamke Asiye Na Mpango Wa Kuendelea Kuwa Nawe Anapokuwa Amekutongoza
Na Pengine Mmekutana Mara Moja Au Mbili, Atakutaarifu Kwa Kuendelea
Kuwasiliana Na Mpenzi Wake Wa Zamani.
Kwa Hakika, Hakuna Jambo Ambalo Humsahaulisha Mwanamke/Mwanaume Mpenzi Wa Zamani
Kama Kumpata Mpenzi Mpya Anayempenda Kwa Dhati.
Iwapo Ataendelea
Kuwasiliana Na Kuzungumza Na Mpenzi Wake Wa Zamani, Hiyo Ni Ishara Kuwa
Hajamalizana Na Mpenzi Wake Huyo Wa Zamani Na Pengine Bado Anatarajia
Kurudiana Naye. Lakini La Muhimu Zaidi Ni Kwamba, Mwanamke/Mwanaume Huyu
Hakupendi Kama Unavyodhani Na Wala Hajawa Tayari Kuwa Nawe Kama Mpenzi
Au Mchumba.
4.HAKUTAMBULISHI KWA MARAFIKI
Mwanaume/Mwanamke Akikupenda, Hususan Vijana Katika Zama Hizi, Lazima Tu
Atakutambulisha Kwa Marafiki Zake, Maana Atakuwa Anajisikia Fahari Kwa
Kufanya Hivyo, Hususan Kama Anahisi Wewe Ni Mwanamke/Mwanaume Maridadi.
Kwa Hulka, Lazima Tu Kijana Wa Kiume/kike Atataka Kujionesha Kwa Watu
Anapokuwa Na Kimwana/mkaka Maridadi Na Anayempenda Kwa Dhati.
Usipoona Dalili
Zozote Za Jambo Hili, Basi Chukulia Tu Kuwa Kijana Huyu Wa Kiume/kike
Hajakupenda Kama Unavyodhani.
5.HUEPUKA WATU KUWAONA PAMOJA
Mwanaume/Mwanamke Asiye Na Mpango Wa Kuendelea Kuwa Nawe Katika Uhusiano,
Hujitahidi Kuepuka Watu Kuwaona Pamoja.
Ni Kweli Kuwa Si Vijana Wote Wa
Kiume/kike Wanaopenda Mapenzi Ya Maonesho Ya Kushikana Mikono Wanapotembea,
Lakini Kama Ameridhika Nawe Lazima Tu Kwa Kiasi Fulani Atataka Umma
Ujue.
Kwa Hakika, Kijana Wa Kiume/kike Anapokuwa Amempenda Msichana/mvulana Kwa Dhati,
Hujikuta Akifanya Hata Mambo Ambayo Zamani Alikuwa Hadhani Kuwa Anaweza
Kuyafanya, Ikiwa Ni Pamoja Na Kuonesha Mapenzi Hadharani, Japo Kwa
Ishara Ndogo Ndogo.
Kwa Tamaduni Za Magharibi Ni Kawaida Kumbusu Mpenzi
Hadharani Au Kumzungushia Mkono Kiuononi, Au Kumshika Mkono, Au Kumbusu.
Lakini Afrika Hata Kutoka Naye Nje Mkizungumza Huwafanya Watu Washuku
Jambo. Kama Hukuliona Hilo Kwa Mpenzi Wako, Basi Chukulia Tu Kuwa
Unapoteza Muda.
6.HAZUNGUMZII MIPANGO YA BAADAYE
Unapokuwa Unazungumza Na Mwanamume/Mwanamke Ambaye Ana Mpango Wa Kuwa Nawe Katika
Kipindi Chake Cha Maisha Yaliyobaki, Lazima Tu Utambaini Akiingiza
Mambo Yanayohusiana Na Maisha Ya Baadaye Mkiwa Pamoja.
Kwa Hakika,
Utambaini Mwanamume/Mwanamke Huyu Akitumia Nafsi Ya Kwanza Wingi Tena Katika Muda
Wa Baadaye, Yaani Akizungumza Mambo Ambayo Atafanya Na Wewe Miaka
Ijayo.
Iwapo Atazungumzia Klabu Fulani Aliyoiona Karibuni Lakini Akawa Hagusii
Kuwa Mtakwenda Huko Siku Moja – Tena Mbaya Zaidi Akawa Anasema Kuwa Huwa
Anakwenda Pale Mara Kwa Mara, Basi Tambua Kuwa Hauko Katika Mipango
Yake Ya Baadaye.
7.HAKUNA MATENDO YA MAHABA
Mwanaume/Mwanamke Asiye Na Mpango Wowote Na Wewe Si Aghalabu Kukufanyia Jambo
Ambalo Utaliona La Kimapenzi Au La Kimahaba, Hususan Anapokuwa
Amefanikiwa Kufanya Mapenzi Na Wewe. Ukiona Hivi, Shtuka Mapema Na Anza
Kuangalia Ustaarabu Mwingine.
Haina Maana Kuwa Asipokununulia Maua Basi Hana Mpango Nawe, Lakini
Angalau Mara Moja Moja Akufanyie Jambo Au Angalau Atoe Kauli Ambayo
Itakusisimua Na Kukufanya Ujione Wa Thamani Na Wa Pekee Machoni Pake.
8.MIPANGO UNAPANGA WEWE
Iwapo Utabaini Kuwa Asilimia 80 Ya Mambo Mnayofanya Pamoja Unayaanzisha
Wewe, Basi Una Kila Sababu Ya Kuutilia Shaka Mustakabali Wa Uhusiano
Wenu.
Kama Ilivyobainishwa Awali, Mwanamume/Mwanamke Akikupenda Atataka Muwe Pamoja
Muda Mwingi, Lakini Kama Utabaini Kuwa Mipango Mingi Unaanzisha Wewe Na
Unazungumza Naye Kwenye Simu Ijumaa Na Mnamaliza Bila Mwanamume Huyu
Kuonesha Dalili Za Kutaka Kuwa Nawe Wikiendi, Japo Kwa Kinywaji, Basi
Chukulia Kuwa Mwanamume Huyu Hana Nia Yoyote Ya Kuwa Nawe Kwa Muda Mrefu
Zaidi.
9.HANA MPANGO NA WATU WAKO
Mwanaume/Mwanamke Anayekupenda Atajishughulisha Na Mambo Yanayohusiana Na Watu
Wako Wa Karibu, Hususan Ndugu, Jamaa Na Marafiki Zako.
Iwapo Utabaini
Kuwa Mwanamume Huyu Haulizi Swali Lolote Kuhusiana Na Familia Yako Au
Marafiki Zako, Basi Tambua Kuwa Hana Mpango Wowote Wa Maana Na Wewe.
Kumbuka Mwanamume Akikupenda Hujaribu Kuwafahamu Na Kuwapenda Watu Wako,
Maana Amependa Boga Na Sheria Ni Kwamba Lazima Upende Na Ua Lake.
10.HAKUMBUKI LOLOTE LA MAANA
Ni Wazi Kuwa Hujakaa Sana Na Mwanaume/Mwanamke Huyu, Lakini Angalau Kuna Mambo
Muhimu Umefanya Naye Ambayo Anapaswa Kuyakumbuka.
Kama Hawezi Kukumbuka
Tarehe Muhimu Za Uhusiano Wenu, Mathalani Tarehe Mliyokutana Mara Ya
Kwanza, Au Siku Mliyofanya Mapenzi, Basi Yamkini Mwanamume/Mwanamke Huyu Hana
Mpango Wowote Wa Dhati Wa Kuendelea Kuwa Nawe.
Ni Matumaini yangu Kuwa uko Sambamba Na Mimi Yaaani... uwe na muda Mwema...
Gonga Like, comment na share kama umeipenda...!!
0 comments:
Post a Comment