Thursday, January 1, 2015

URUSI YAKABILIWA NA MFUMUKO WA BEI

URUSI inakabiliwa na mfumuko wa bei uliofikia asilimia 11.4, katika kipindi cha mwaka 2014 kutokana na kuporomoka kwa thamani ya fedha ya nchi hiyo.
Serikali ya urusi imesema kuwa Kuanguka kwa thamini ya fedha katika nchi hiyo kumechangia bei kupanda ikiwemo bei ya vyakula iliyopanda  hadi kufiki asilimia 15.4 kwa mwaka.
Hata hivyo kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa nchini humo  bei ya chakula ilipanda kwa asilimia 2.6 katika kipindi cha mwezi Desember kutokana na mporomoko wa thamani ya fedha nchini humo.
Mwaka 2013 mfumko wa bei ulipanda hadi kufikia asilimia 6.5 ambapo mwaka 2014 umeonekana kupanda zaidi tangu nchi hiyo ikubwe na mgogoro wa kifedha kuanzia mwa 2008.
Kushuka kwa bei ya mafuta kumepelekea kushuka kwa pato la serikali ya urusi, lakini pia vikwazo iliyo wekewa nchi hiyo dhidi ya Ukraine vimepelekea sekta ya bank kutopata mikopo ya kigeni.
LIKE PAGE YETU KUFUATILIA MATUKIO ZAIDI.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI