Ndumbagwe Misayo ‘ Thea’ |
KAMA Waswahili wasemavyo ukubwa ni dawa, basi hilo limedhibitika siku ya Ijumaa Boxing day pale kundi jipya linaundwa na wakongwe wa tasnia ya filamu Swahilihood lijulikanalo kwa jina la Kaone Sanaa Group lilipozindua tamthilia yake mpya na ya kusisimua ya Kipusa na kuonyesha uwezo wa hali ya juu.
Uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala na kuonyesha ngoma za asili kwa umahiri mkubwa kabisa na mgeni wa heshima alikuwa ni Mh. January Makamba Mbunge wa Bumburi, kundi la Kaone Sanaa Group ni mbadala wa kundi la Kaole Sanaa Group kwani wasanii wanaounda kundi hili ni kutoka hilo.
Kundi la Kaone Sanaa Group linaundwa na wasanii mahiri katika tasnia ya filamu Bongo ambao ni Ndumbagwe Misayo ‘Thea’, Rashid Mzange ‘Kingwendu’, Abdalah Mkumbilah ‘Muhogo Mchungu’, Issa Kipemba ‘Kipemba’, Adam Melele ‘Swebe’, Shamira Ndwangila ‘Bi. Staa’, Halima Yahaya ‘Davina’, Dora Redson ‘Kadada’, Colleta Raymond.
Wengine ni Bahati Hassan ‘Iman’, Madina Khamis ‘Zawadi’, Nia Justine ‘Nia’, Eva Clemence ‘Subira’, Pili Lwey ‘Mama Kibakuli’, Happiness Stanslaus ‘Nyamayao’, Juma Watuta ‘Chapu chapuo’ Hadija Mohamed ‘Bi. Fety’ na wengineo wengi wakali katika tasnia ya filamu Swahilihood.
Makamba akizungumza |
Akiongea na FC kiongozi wa kundi hilo Ndumbagwe Misayo ‘ Thea’ amesema kuwa kundi hilo limekusudia kutuliza kiu ya watanzania kukosa tamthilia zenye maadili zilizokosekana kwa muda mrefu toka wao waondoke katika uigizaji katika televisheni.
“Kaone Sanaa Group ndio jibu sahihi ya kiu cha muda mrefu kwa wapenzi wa tamthilia baada ya kukosekana kwa muda mrefu, sasa tumerudi kukonga nyoyo zao, kulinda maadili ambayo imekuwa ni kilio cha baadhi ya watazamaji wengi,” anasema Thea.
0 comments:
Post a Comment