
UPO
msemo uliotawala vichwa vya watu tangu dahari kwamba wanawake ni tabaka
la kukaa nyumbani na kufanya kazi za ndani. Wao jukumu lao ni
kumfurahisha mume na lingine ni kuwaandaa watoto kwa ajili ya kwenda
shule na kufuatilia nyenendo zao darasani.
![]() |
Happiness Magesse.
|
Ilivyozoeleka
ni kwamba wanawake ni goigoi. Utaona bungeni kuna wabunge wa viti
maalum ambavyo wengi hutafsiri kuwa ni vya upendeleo. Kwa maana kwamba
uwezo wao kushindana kwenye majimbo na kushinda ni mdogo ndiyo maana
wanapewa hivyo maalum kwao.
Katika
mitihani, kuna unafuu wa alama za ufaulu kwa wanafunzi wa kike. Yaani
wanaonekana hawana uwezo wa kushindana na wavulana. Vijijini, wanawake
wamekuwa wakitumika kama nyenzo ya kilimo, yaani mama akalime ndiyo
alishe familia, baba akacheze bao au kunywa pombe.
Miaka
inakwenda, wapo wanawake wengi ambao wameweza kudhihirisha kwamba
inawezekana kwa jinsi ya kike kuanzisha kazi na kufanikiwa. Aliyekuwa
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro ni mfano
wenye nguvu kwa wanawake kufanikiwa.
Spika
wa Bunge, Anne Makinda, Mchungaji Getrude Rwakatare na wengineo, ni
kichocheo kinachotoa uthibitisho kuwa wanawake wanaweza. Ni suala la
kuwaamini na kuwapa nafasi, kwa hakika wanaweza kufanya mambo makubwa
mno.
Ukiachana
na hao, ipo orodha ya wanawake vijana 10 ambao wanastahili pongezi.
Wamepambana katika maeneo yao kiasi cha kupata mafanikio ambayo
yameonesha njia. Inabidi tuwatambue na kuthamini jitihada zao kwa maana
wameendelea kuthibitisha ndivyo sivyo kwa wale waliokuwa wanaamini kuwa
wanawake si lolote kwenye utafutaji.

FLAVIANA MATATA
Mwaka
2007 alipokwenda kushiriki mashindano ya dunia ya Miss Universe na
kushika nafasi ya sita, wengi walidhani huo ndiyo mwisho wake.
Ilionekana hivyo kwa sababu warembo wengi wameshiriki mashindano ya
dunia na baada ya kurudi nchini, hawakusikika tena.
Kwa
Flaviana, huo ulikuwa ni mwanzo wa kupiga hatua zaidi kusaka mafanikio
yake. Hivi sasa, mrembo huyo ni mwanamitindo wa kimataifa, anayefanya
kazi na makampuni makubwa ulimwenguni.
EMELDA MWAMANGA
Ni
mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Relim
Entertainment inayomiliki jarida maarufu la Kiingereza, Bang. Jinsi
alivyoweza kulisimamisha jarida hilo na kulifanya kuwa maarufu zaidi
nchini, inatosha kumpongeza kwamba ameonesha.

Jina
lake asilia ni Judith Wambura. Ni mwanamuziki wa kike mwenye mafanikio
zaidi ambayo chanzo chake ni muziki. Anamiliki bendi na mgahawa wa
kisasa ambao ulimgharimu zaidi ya shilingi milioni 100 kuuanzisha. Bila
shaka Jaydee ameonesha njia kwa wanamuziki wengine wa kike hapa nchini.
MADAM RITA
Kuanzisha
kitu wakati mwingine inaweza kuwa jambo rahisi lakini uimara wa mtu ni
pale anapoweza kulisimamia na kufanikiwa. Rita Paulsen anastahili
pongezi kwa namna alivyoweza kuanzisha Shindano la Bongo Star Search na
kulifikisha hapa lilipo. Huyu ni mwanamke kijana aliyeonesha njia ya
kweli ya mafanikio.
RAHMA AL-KHAROOS
Anamiliki
Kampuni ya RBP Oil & Industrial Technology. Uwezo wake uliweza
kuwashtua wengi pale alipoweza kujitolea mamilioni ya fedha kuiwezesha
Timu ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars. Mwanamke huyu ni mfano tosha
kwamba inawezekana kama tu utaamua kupambana.

SHEAR NASSA
Anamiliki
maduka ya Shear Illusions, vilevile ana jarida linaloitwa Shear Hair
& Beauty. Ukubwa wa maduka yake, heshima na umaarufu wake kwa uuzaji
wa vitu vya urembo ni kielelezo cha kumthibitisha Shear kwamba ni
mwanamke kijana aliyefanikiwa, kwa hiyo ameonesha njia.

KHADIJA MWANAMBOKA
Mbunifu
wa mavazi wa kike mwenye umaarufu kuliko wanawake wote nchini. Ameanza
harakati zake akiwa na umri mdogo na kwa alipofikia hivi sasa,
ameshaonesha njia kwa wanawake wengine nchini. Jambo muhimu ni kusimamia
fani yako mpaka kuifikisha kwenye kiwango bora. Khadija alipofikia kwa
ubunifu wa mavazi, anastahili pongezi

FINA MANGO
Alipata
umaarufu mkubwa kwenye fani ya utangazaji wa redio lakini alipoamua
kuanzisha kampuni yake ya One Plus, ameweza kupata mafanikio makubwa.
Tenda ya kuratibu na kusimamia Tuzo za Muziki Tanzania (Tuzo za Kili)
kwa miaka mitatu mfululizo imedhihirisha ubora wa kampuni yake

Huyu
ni mama Asha Baraka mkurugenzi ASSET hakika ni mpiganaji
sana wa maendeleo ameweza kuwaajiri vijana wengi sana
kupitia kampuni yake ya Asset ambayo inamiliki bendi ya
twanga pepeta. licha hivyo ASHA BARAKA maaarufu kama
iron lady ameweza kusaidia vijana wengi kupata mafanikio
ya mziki kupitia bendi yake twanga pepeta
0 comments:
Post a Comment