WAKATI napita pita katika mtandao nikawa natafuta makala mbalimbali za namna ya ugonjwa huu wa kukoroma unavyotokea na jinsi ya kuweza kuudhibiti kwa mtu mwenye tatizo. Nimesoma makala nyingi nikaja kukutana na makala moja ambayo kwa maelezo yake na jinsi watu walivyofuata maelekezo tatizo ilo limeweza kuondoka nikiwemo mimi mwenyewe mwandishi.
Hatua za kufanya katika kulitibu tatizo; cha kwanza kinachofanyaka ni mazoezi tu na sio dawa za mitishamba au hospitali.
Hatua ya kwanza: Fungua mdomo wako wazi:
Hatua ya pili: Toa ulimi wako nje ukiwa umeacha mdomo wazi, usukume ulimi mpaka mwisho utahisi maumivu mwishoni mwa ulimi.
Hatua ya tatu: urudishe ulimi ndani kwa kuukunja kwa mbele. Baada ya hapo sasa zoezi linakuwa ni kutoa ulimi na kurudisha ndani mara 20 ukimaliza mara ya kwanza unapumzika tena unafanya kwa safari tatu kwa siku.
Zoezi hili la kutoa ulimi nje na kurudisha ndani kwa safari moja unahesabu mara 20 halafu unapumzika na kurudia tena safari mbili zilizobaki kwa muda mwingine hivyo kwa siku ni mara tatu ambapo utafanya mara 60 kutoa ulimi nje na kurudisha kwa ujumla wa hawamu zote hizo tatu. Utafanya kwa siku 10
Baada ya kuanza zoezi hili utaanza kupata mabadiliko madogo madogo kwanzia ndani ya siku tatu.
0 comments:
Post a Comment