“…Nilitukanwa sana jana kwa kuwish wenzangu
kheri ya xmass na kuonekana sina dini... Niseme kitu kimoja wasanii
kwenye mitandao hatupo kwa ajili ya kutangaza dini tupo kwa ajili ya
kutangaza kazi zetu na kuwa karibu na nyinyi mashabiki wetu.
Pili kazi yangu hainunuliwi na watu wa dini
moja tu mi nafikiri uvivu wa kufikiri na wepesi wa kusahau kuwa msanii
ni nani ndio unawafanya maneno mengi yawatoke, mi msanii sio mwana zuoni
msinivike taji lisilo kuwa langu, kama mahodari
wa kufundisha watu dini basi katazeni na viongozi wenu wa kislam
wasijumike na watu wakatazeni na kina Salmankhn wa India ambao
wamemaliza misahafu lakin wanavaa kofia za xmass, Je kazi zetu
zingenunuliwa kwa ajili ya dini, tungekuwa wapi leo?
Nina follows
zaidi ya elfu 96 sidhani kama wote ni dini yangu, kifupi sipendi
malumbano ya dini kwenye page yangu plz naheshimu kila mtu na kila
shabiki yangu hata kama mpagani ukitukana tu hapa mi na wewe..” -
Wastara Sajuki
Huu si uungwana jamani, udini sio ishu! Tubadilike.
0 comments:
Post a Comment