Thursday, November 6, 2014

WANAJESHI WA LIBYA WALIOJIHUSISHA NA VITENDO VYA NGONO, WAFUKUZWA NCHINI UINGEREZA… SOMA HAPA!

Wanajeshi kutoka nchini Libya wamerejeshwa nchini kwao kutokana na kukosa uadilifu wakiwa mafunzoni Uingereza huku wengine wakituhumiwa kufanya vitendo vya ukatili.
WANAJESHI hao waliokuwa mafunzoni nchini Uingereza, 300 kati yao wamesharejeshwa Libya kutokana na tuhuma kuhusiana na unyanyasaji wa kimapenzi.

Waziri wa Ulinzi wa Libya amethibitisha kurejeshwa kwa askari hao na kuongeza kuwa wengine watarejeshwa siku chache zijazo.
wanajeshi wawili wa Libya wamekiri kufanya vitendo vya unyanyasaji wa kingono dhidi ya wanawake huko Cambridge, ambapo wawili wameshafikishwa mahakamani wakikabiliwa na mashitaka ya ubakaji.

Baadhi ya wakazi wa eneo jirani na kambi ya jeshi walipo wanajeshi hao wa Libya,wamesema kuwa wamekuwa wakiwaona wanatoka nje ya ngome za jeshi kwaajili ya kununua pombe, na tayari waziri wa ulinzi amekiri kupokea mashtaka hayo na kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya wanajeshi hao wa kigeni.

Waziri huyo wa Libya amesema wanajeshi hao wanaruhusiwa kutoka nje ya kambi kwa saa tatu pekee kwani madhara ya askari hao kuzurula mitaani ni makubwa na wengine hujitumbukiza katika matumizi ya dawa za kulevya na ulevi wa kupindukia.

MWISHO.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI