Tuesday, November 18, 2014

CHADEMA YAFUNIKA KWA MKUTANO WA KIHISTORIA *PICHAZ*

Na Mohamedi Mtoi
MWENYEKITI Taifa amefanya mikutano mitano kwenye majimbo matatu ya Ulanga Magharibi, Ulanga Mashariki na Kilombero.
Mikutano yote ilikuwa mikubwa sana na yenye hamasa kubwa huku wenyeviti saba wa CCM wa vijiji kwenye jimbo la Ulanga Mashariki wakirudisha kadi za CCM na kujiunga na CHADEMA na kuahidi kuongeza nguvu zaidi kwenye Operation Delete CCM ambapo watasaidia wagombea watakao simamishwa na Chadema pamoja na vyama vingine vya UKAWA.
Kesho itafanyika mikutano minne ambapo mkutano wa mwisho utafanyika jimbo la Morogoro mjini na kuhitimisha ziara ya mwenyekiti wa chama Taifa (Mh Mbowe); baada ya mwenyekiti Taifa kuhitinisha ziara mkoa wa Morogoro, katibu mkuu wa chama (Dr slaa) atampokea kijiti na kuendeleza ziara ya kanda ya kati kwenye mikoa ya Dodoma na Singida.
Ziara za chama ndio zimeanza rasmi na zitakuwa endelevu bila kukoma mpaka 2015.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI