Tuesday, November 18, 2014

“BAHARI ISHACHAFUKA NDUGU ZANGU NTAFUTIENI MFUKO NITAPIKE" SABABU INAYOMFANYA DIAMOND ATAMANI KUTAPIKA IKO HAPA!!!

DIAMOND Platnumz alipata A kwenye somo la kucheza na akili ya mashabiki wake. Siku za hivi karibuni staa huyo amekuwa akitease mashairi ya kile kinachoonekana kama wimbo wake ujao.
Na sasa amewapa mashabiki wake kitu kingine.. picha inayoonekana kuwa ni video yake mpya.

Hicho ndicho kitu pekee ambacho staa huyo huwa hatua 100 mbele zaidi ya wasanii wengi katika kazi zake. Kupitia Instagram na Facebook, Diamond amepost picha akionekana akicheza muziki na model mrembo wa kizungu. Hakuna shaka kuwa hii ni video yake mpya.
“Bahari ishachafuka ndugu zangu ntafutieni mfuko nitapike,” ameandika kwenye picha hiyo.
Alishoot lini na wapi? Hilo ni swali lenye majibu ya kukisia tu. Kisio sahihi linaweza kuwa video hiyo alishoot Afrika Kusini kipindi kile kile aliposhoot video ya wimbo alioshirikishwa na msanii wa Nigeria, Waje.
Kwakuwa ameamua kuyapeleka mambo yake kisiri kwa sasa, ndio maana huenda hakupost picha yoyote kuonesha kuwa ameshoot video mpya. Lakini kwa picha hii ya sasa, huenda Diamond akatusurprise kwa mara nyingine tena!

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI