MWANAMUME yeyote
anapotaka kumtongoza mwanamke hulazimika kwanza kumwonesha – japo kwa matendo –
kuwa anampenda, au kwamba amevutiwa naye, hata kama ni kimwili tu. Hatua hii
ndiyo yenye changamoto kubwa zaidi kwa mwanamume, maana ndipo wakati anapokuwa
anajaribu kufikisha ujumbe kwa mlengwa huku yeye mwenyewe akijihakikishia kuwa
haharibu mambo.
Mwanamume
anapokuwa anajaribu kufikisha ujumbe wa “nakupenda” kwa mwanamke, mapigo ya
moyo yanaweza kumwenda mbio, hususan kama mwanamke mwenyewe anaonekana kuwa
“maji marefu”. Hata hivyo, ni kazi ambayo kila mwanamume hulazimika kuifanya.
Kazi hii ya
kufikisha ujumbe kwa mara ya kwanza
huhitaji umakini. Bahati njema, shughuli yenyewe ina sayansi yake, ambayo ina
misingi katika mahusiano ya kijamii. Ukifahamu sayansi hii inaweza kuwa rahisi
zaidi kwako kufikisha ujumbe kwa mtarajiwa wako – na kufanikiwa.
1. KUKUTANISHA
MACHO NI MUHIMU
Kawaida, mambo
yote huanzia – na pengine kuishia – katika kukutanisha macho. Mwanamke
atakapobaini kuwa hujajaribu kumwangalia japo kwa sekunde mbili mfululizo,
ataondoa mawazo na hisia zake kwako hata kabla hujasema neno lolote.
Macho ndizo
zana muhimu zaidi mtu anapokuwa anataka kufikisha ujumbe kwa mwenzake kuwa
anampenda, au amevutiwa naye. Hii ni kwa sababu macho ndiyo vipitisho na
visambazaji muhimu vya ishara baina ya mtu na mtu, hata kama si katika masuala
yanayohusiana na mapenzi.
Kukutanisha
macho na mtu wa jinsia nyingine unayevutiwa naye au anayevutiwa nawe ni jambo lenye nguvu za ajabu katika kuanzisha uhusiano.
Kwa sababu hiyo, hata unapofanikiwa kumtazama moja kwa moja machoni mwenzako
hutarajiwi kutumia zaidi ya sekunde mbili, kutokana na nguvu iliyomo katika
mawasiliano haya.
Katika hili,
wanaume mahiri hufahamu ni wakati gani wa kumwangalia mwanamke na ni wakati
gani wa kutomwangalia. Mara nyingi, ni vizuri zaidi kumwangalia zaidi mwanamke
wakati anapozungumza, huku ukikwepesha macho kidogo pale unapozungumza wewe.
2. UNATAKIWA
UWIANO, UKWELI KATIKA MAZUNGUMZO
Ni jambo
lisilopingika kwamba wanaume na wanawake wanatofautiana katika maana ya dhana
ya mawasiliano. Hata hivyo, bado inawezekana kuendesha mazungumzo shirikishi na
yenye kuburudisha ukiwa na mwanamke, bila kuonekana wa bandia.
Watu wa jinsia
zote mbili wanaweza kutuhumiwa kwa kupindisha ukweli na kujaribu kuficha tabia
na mienendo yao wanapozungumza na wapenzi watarajiwa. Naam, katika mazungumzo
ya kwanza baina ya wapenzi au wachumba watarajiwa uwongo – ukiwemo ule
usiotarajiwa – huwa mwingi.
Katika
mazungumzo ya kwanza ni kawaida kwa mwanamume kubadilisha matendo yake na
mtindo wake wa kuzungumza kwa maslahi ya kumpata mwanamke, jambo ambalo
huifanya hulka yake ya wakati huo kuwa ya bandia.
Lakini pia wasichana/wanawake
husema “Nakupenda” bila kumaanisha, pengine kwa ajili ya kumfurahisha
mwanamume, au kusikia mwanamume atasemaje.
Jambo la
muhimu katika mazungumzo ya awali baina ya mwanamume na mwanamke ni kuepuka
michezo ya kudanganyana na kukwepana, badala yake, yafanye mazungumzo kuwa
rahisi na halisi. Hapo ndipo mwanamume hujitofautisha na wanaume wengine na
kupendwa kwa sababu hiyo.
3. USIPUUZE
NGUVU YA LUGHA YA MATENDO
Wakati mtu
anapokuwa akijaribu kuwasilisha ujumbe wa “Nakupenda” kwa mwenzake, lugha ya
matendo yake huzungumza kwa sauti kubwa zaidi kuliko maneno yake. Hili limeweza
kuthibitishwa kwa nyakati mbalimbali kutokana na tafiti mbalimbali.
Katika
muktadha wa kujaribu kufikisha ujumbe wa “Nakupenda” kwa mlengwa, lugha ya
matendo ndiyo yenye nafasi kubwa zaidi. Kwa hakika, asilimia kubwa ya ujumbe
unaowasilishwa kwa mlengwa huwasilishwa kwa njia ya matendo ya mwili na si
maneno. Ni asilimia ndogo tu ya ujumbe inayowasilishwa kwa maneno – na wakati
mwingine maneno huweza kuleta matatizo maana katika kuzungumza kuna kujikwaa
kwingi, kwani ulimi hauna mfupa.
Ili uweze
kufanikiwa katika kueleza nia yako kwa mwanamke, lazima ujue jinsi ya kutumia
lugha ya matendo yako. Na pengine hutatumia nguvu, maana watu husema penzi
kikohozi – kama unalo litaonekana tu machoni pa mlengwa.
Ukitafakari
kwa makini utabaini kuwa huhitaji kusema sana ndipo uweze kupendwa, kwani
maneno huchangia asilimia kidogo tu. La muhimu ni kuhakikisha kuwa mlengwa wako
anakusoma na kukuelewa vizuri kwa kuangalia matendo ya mwili wako.
4. ACHA ASILI
ICHUKUE MKONDO WAKE
Katika
nadharia mbalimbali za kijamii na kidini ni jambo la kawaida kusikia kuwa
binadamu wote ni sawa. Hata hivyo, katika muktadha wa kimapenzi, kila mtu mmoja
mmoja anafahamu kabisa kuwa si kila mwanamume/mwanamke ni sawa na mwenzake.
Methali yenye
asili ya kimagharibi husema “Uzuri wa mtu uko katika macho ya yule
anayemtazama.” Hii ina maana pia kwamba, kila mtu anavyo vigezo vyake vya uzuri
kwa kuzingatia maumbile yake. Pia jamii zinavyo vigezo vya uzuri, lakini
hutangulia kwanza vigezo binafsi.
Unapokuwa
umekaa na mwanamke ambaye anakuvutia kwa mwonekano wake, sauti yake na
kadhalika, si rahisi sana kujizuia kuonesha kuwa anakuvutia. Hii ni kwa sababu
si wewe, bali ni nafsi yako inayokusukuma. Na yeye mwenyewe atakusoma kwa
kuangalia lugha ya matendo yako na kukwelewa, utakaobaki ni uamuzi wake tu.
Katika jamii
kuna vigezo kuhusiana na kiuno, miguu, maziwa, makalio na kadhalika. Wengi wa
wanajamii huvizingatia na kuongeza vyao. Huu ni ukweli wa kibiolojia ambao
hauwezi kupingika. Mwanamke mwenye vigezo vinavyokubalika zaidi katika jamii
yake atawavutia wanaume wengi zaidi. Hapa mwanamume hahitaji kutumia nguvu
nyingi – asili ya maumbile itamsaidia humtambulisha mwanamke kuwa amempenda.
5. TUMIA
CHANGAMOTO YA WALAKINI
Mara nyingi
changamoto kubwa katika suala zima la mtu kubainisha nia yake kwa mwanamke
hutokana na ukweli kwamba katika mchakato mzima huwa kuna wasiwasi na walakini.
Kwa hakika, jambo hili ni la “pengine” au “labda” kutokana na kutoweza kufahamu
kirahisi mwenzako anawaza nini.
Unapoonesha
nia yako ya kumpenda mwanamke, ni kama unaamsha hisia zake kwako na ni kama
vile unamuuliza: “Ungependa kuwa nami?” Kwa njia hii ni kama utakuwa unafungua
mlango wa kupata jibu la “ndiyo” au “hapana” kwani huyo unayemwonesha kuwa
unampenda na yeye ana matakwa yake na mapendeleo yake.
Kimsingi
hakuna kanuni wala sheria rasmi unazopaswa kuzingatia wakati wote. La muhimu ni
wewe mwenyewe kujiachia na kuingia katika maji usiyofahamu kina wala mwisho
wake, bali wewe nenda na mkondo wake huku ukitarajia kuwa lolote linaweza
kutokea. Hiyo ndiyo sehemu ya raha yake.
6. DHIBITI
HISIA, MIHEMKO
MWANAMUME
yeyote anapotaka kumtongoza mwanamke hulazimika kwanza kumwonesha – japo kwa
matendo – kuwa anampenda, au kwamba amevutiwa naye, hata kama ni kimwili tu.
Hatua hii ndiyo yenye changamoto kubwa zaidi kwa mwanamume, maana ndipo wakati
anapokuwa anajaribu kufikisha ujumbe kwa mlengwa huku yeye mwenyewe
akijihakikishia kuwa haharibu mambo.
Mwanamume
anapokuwa anajaribu kufikisha ujumbe wa “nakupenda” kwa mwanamke, mapigo ya
moyo yanaweza kumwenda mbio, hususan kama mwanamke mwenyewe anaonekana kuwa
“maji marefu”. Hata hivyo, ni kazi ambayo kila mwanamume hulazimika kuifanya.
Kazi hii ya
kufikisha ujumbe kwa mara ya kwanza
huhitaji umakini. Bahati njema, shughuli yenyewe ina sayansi yake, ambayo ina
misingi katika mahusiano ya kijamii. Ukifahamu sayansi hii inaweza kuwa rahisi
zaidi kwako kufikisha ujumbe kwa mtarajiwa wako – na kufanikiwa.
0 comments:
Post a Comment