MUIGIZAJI
maarufu nchini Wema Sepetu na Mchekeshaji MC Pilipili wanatarajiwa kuwa
wa kwanza kukizindua kipindi cha Kili Chat Shows kinachotarajiwa kuanza
leo. Kipindi hicho kitakachokuwa kikiendeshwa na Gadner G Habash
kitakuwa ni cha nusu saa na kitakuwa kikiwakutanisha mastaa wawili
wanaoshabikia timu za Yanga na Simba ambapo watapata nafasi ya
kushindana namna wanavyozielewa klabu hizo. Pia mashabiki watapata
nafasi ya
kuwahoji maswali kuhusu shughuli zao.Kipindi hicho kitakachokuwa
kikirushwa Alhamisi saa tatu usiku katika kituo cha East Africa TV ni wa
kampeni ya Nani Mtani Jembe ambayo ilianza mwanzoni mwa mwezi huu kwa
mashabiki wa Yanga na Simba kushiriki kampeni hiyo ambayo jumla ya Sh
100 zinashindaniwa kwa mashabiki kupiga kura kwa SMS kwa kutuma namba za
ndani ya kizibo kila wanapokunywa bia ya Kilimanjaro.
0 comments:
Post a Comment