Monday, October 20, 2014

MTI WA MAAJABU TANZANIA: WAANGUKA NA KUINUKA BAADA YA MIAKA 3, YANI KAMA ULIKUWA USINGIZINI VILE! *VIDEO*

Mti unaodaiwa kunyanyuka ghafla baada ya kuanguka miaka mitatu iliyopitakatika kijiji cha Mfuto kata ya Ufuluma, wilaya ya Uyuwi mkoani Tabora.
KATIKA hali ya kushangaza huku kila mtu akifikiria yake baaya ya juzi huko mkoani Tabora, kutokea tukio la aina yake ambapo inaelezwa kuwa mti aina ya Msufi uliokuwa umeanguka yapata miaka mitatu iliyopita umesimama ghafla tena kwa sauti kubwa ya mrindimo na kuwafanya wananchi kujitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo.
Tukio hilo limetokea Oktoba 17,mwaka huu,katika kijiji cha Mfuto kata ya Ufuluma katika wilaya ya Uyuwi mkoani Tabora.
Inaelezwa kuwa mti huo wenye kipenyo cha futi 2 uliinuka na kuwa kama zamani baada ya kutokea upepo mkali katika kijiji hicho.
Wananchi walikusanyika kila mmoja akitaka kuchukua angalau gome la mti huo kwa ajili ya dawa ama kumbukumbu , na haya ndio maajabu ya Tanzania
Angalia video hii ili ushudie maajabu haya!!!

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI