Bilo
(kulia) na muhibu (katikati) wakiwa na daktari wa timu hiyo wakiburudika na
gazeti bora la michezo nchini la championi.
MKURUGENZI
wa Ufundi, Muhibu Kanu na Kocha Msaidizi Athuman Bilali ‘Bilo’ wa Stand
United wameamua kurudi darasani kuongeza ujuzi kwa kusoma kozi kupata
leseni C ya Shirikisho la Soka la Afrika (Caf).
Mkurugenzi
huyo amesema kuwa wameamua kwenda kuongeza ujuzi ili kuwa hodari zaidi
katika kazi yao ya kufundisha kwa sababu wanataka kukiboresha zaidi
kikosi chao kiufundi.
“Tumeamua
kwenda kusoma kuboresha mambo kadhaa katika benchi letu la ufundi, mimi
nitaanza hivi karibuni na kozi yangu nitachukulia mkoani Morogoro na
kocha ameshaanza kusoma yupo Dar es Salaam.
“Kocha
mkuu yupo anaendelea kuinoa timu kama kawaida na kozi zenyewe ni kwa
muda mfupi tu, hivyo baada ya hapo tutarudi na kuendelea kuijenga timu
yetu kama kawaida,” alisema Kanu.
0 comments:
Post a Comment