MAHARUSI wilayani hapa wameacha gumzo baada ya kukodi helikopta kutoka Kenya kunogesha harusi yao na kuruka angani.
Tukio
hilo lilitokea juzi saa 9:00 alasiri katika mji mdogo wa Tarakea uliopo
mpaka wa Tanzania na Kenya. Maharusi hao, Lameck Yesse na Gladmarry
Mushi walivuta hisia za wengi kwa kuwa bwana harusi ni dereva wa gari
dogo la abiria aina ya Toyota Noah analolimiki na bibi harusi ni
mwanafunzi wa chuo jijini Arusha.
Mashuhuda walisema tukio hilo ni la kwanza na la aina yake katika mji huo.
Maharusi
hao walifunga ndoa katika Usharika wa Tarakea wa Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT), na ibada iliongozwa na Mchungaji Emmanuel
Dediok.
0 comments:
Post a Comment