MSHAMBULIAJI wa zamani wa Tottenham ya England ambaye sasa anakipiga
Santos ya Brazil amejikuta akiingia matatani baada ya kujivuta jezi na
kuanguka.
Leandro Damiao alijivuta jezi na kuanguka wakati akiichezea Santos katika Ligi ya Brazil.
Damiao alifanya hivyo akiwa katika harakati za kumshawishi mwamuzi.
Hata hivyo mwamuzi huyo alishitukia mchezo, hakutoa adhabu hiyo ya penati.
Tayari
Shirikisho la Soka la Brazil (CBF) liko katika hatua za kumchukulia
hatua na imeelezwa adhabu yake huenda ikawa ni kufungiwa kucheza mechi
sita za ligi.
0 comments:
Post a Comment