Wednesday, September 17, 2014

UONGOZI WA KAMPUNI YA NYUMBA YA NAKHEEL, AMBAYO NDIO KAMPUNI KUBWA YA SERIKALI DUBAI WATEMBELEA NHC, WAFANYA MAZUNGUMZO

Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai Mhe Omar Mjenga (kulia) akiongozana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Nakheel ambayo ndio kampuni kubwa ya Serikali Dubai ambayo ni wawekezaji wakubwa duniani katika sekta ya uendelezaji miliki, Rashid Ahmed Lootah, kuingia kwenye chumba cha mikutano cha Ofisi za Mkurugenzi Mkuu wa NHC jiji Dar es Salaam jana, nyuma yake ni Mkurugenzi Mkuu wa Ujenzi wa Miradi wa Kampuni hiyo, Masood Al Zarooni na Injinia Fawzi Al Shah ambaye ni Mkurugenzi wa Udhibiti na Mipango Miji wa Kampuni hiyo.
Mwenyekiti huyo na ujumbe wake wakiongozwa na Balozi Mjenga walikuwa na mazungumzo na Menejimenti ya Shirika la Nyumba la Taifa kuhusiana na fursa za uwekezaji zilizopo katika Satellite Cities na Fursa za Kujenga uwezo wa masuala mbalimbali katika uendelezaji miliki. Baadhi ya miradi iliyosimamiwa na kampuni hiyo ni pamoja na The Palm Dubai (the largest island Palm City in the World), Nakheel Mall, Dragon Mart na baadhi ya hotel za nyota tano Jijini Dubai.
 Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai Mhe Omar Mjenga (kulia) akiongozana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Nakheel ya Dubai ambayo ni moja ya wawekezaji wakubwa duniani katika sekta ya uendelezaji miliki, Rashid Ahmed Lootah, nyuma yake ni Mkurugenzi Mkuu wa Ujenzi wa Miradi wa Kampuni hiyo, Masood Al Zarooni na Injinia Fawzi Al Shah ambaye ni Mkurugenzi wa Udhibiti na Mipango Miji wa Kampuni hiyo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akimkaribisha Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai Mhe Omar Mjenga
   Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akimkaribisha Injinia Fawzi Al Shah ambaye ni Mkurugenzi wa Udhibiti na Mipango Miji wa Kampuni hiyo ya Nakheel.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Kampuni ya Nakheel ya Dubai, Rashid Ahmed Lootah na Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai Mhe Omar Mjenga.
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Kampuni ya Nakheel ya Dubai, Rashid Ahmed Lootah na Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai Mhe Omar Mjenga.
 Uongozi wa Kampuni ya Uendelezaji Miliki ya Dubai, Nakheel ukiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Shirika la Nyumba la Taifa kwenye makao makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa, jijini Dar es Salaam.
Uongozi wa Kampuni ya Uendelezaji Miliki ya Nakheel ukiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Shirika la Nyumba la Taifa kwenye makao makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa,  jijini Dar es Salaam.
Uongozi wa Kampuni ya Uendelezaji Miliki ya Nakheel ukiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Shirika la Nyumba la Taifa kwenye makao makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa,  jijini Dar es Salaam.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI