Monday, September 29, 2014

JINSI UGONJWA WA UTI UNAVYOWEZA KUPOTEZA MAISHA YAKO

MAAMBUKIZI Katika Njia ya Mkojo (UTI) ni moja kati ya magonjwa ambayo hayapewi msisitizo wa kutosha katika jamii licha ya kuwa wengi huathirika kwa ugonjwa huu bila kujua chanzo, tiba na kinga yake.
Ugonjwa huu huanza kuathiri mirija inayopitisha mkojo, baadaye huenea katika kibofu na figo. Mgonjwa anaweza kupata ugonjwa sugu wa figo na kupoteza maisha kama ugonjwa huu hautatibiwa mapema.
Wataalamu wa afya wanasema UTI husababishwa na vimelea ambao huingia kupitia mirija inayosafirisha mkojo na kuutoa nje. Vimelea hawa wanashambulia kibofu na baadaye huendelea mpaka kwenye figo. Hii ndiyo hatua kubwa ya ugonjwa ambayo inaweza kusababisha kifo au tatizo la kudumu.
Hawa ni vimelea wa jamii ya bakteria walio wanajulikana kwa jina la escherichia coli (E.coli).
Bakteria hawa wanapatikana katika utumbo mpana lakini husafiri kupitia njia ya haja kubwa kwenda katika njia ya mkojo na kusababisha maambukizi katika kibofu na figo.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI