Monday, September 29, 2014

HATIMAYE DIAMOND AFUNGUKA YAKE YA MOYONI...ATOA UTATA ULIOPO KWA MASHABIKI WAKE KUHUSU MENINAH

Hatimaye Diamond Platnumz amefunguka kuhusu tetesi zinazoendelea kuwa ameachana na Wema Sepetu na kwamba ana mpango wa kufunga ndoa na Meninah Diamond alisema kuwa tetesi hizo zimekuwa zikimhuzunisha kwa kiasi kikubwa. “Unajua hizi habari kiukweli zimekuwa zikinihuzunisha sana,” amesema msanii huyo. “Unajua mie ni mtu mmoja ambaye sipendi kuzunguzia mambo ya rumors, siju magazeti huwa sipendi kuzungumzia kabisa, kwa kuwa najua kabisa siwezi kubishana na media kwakuwa media ni kubwa, maana najua utaongea na huyu na yule siku ya siku utagombana na watu. Ndio maana huwa nakaa kimya,” ameongeza “Kusema ukweli hili suala limekuwa likiniumiza ‘eti sijui kuna vikao vya harusi mie nataka kumuoa Meninah’ Kusema ukweli sina mahusiano na Meninah. Kila mtu anajua mie nina mahisiano Wema. Wema ndo mpenzi wangu, ila wakati mwingine nakuwa naelewa ile inakuwa ni trick ya kibiashara. Mtu anajua hata nikimuandika vipi ‘Diamond sijui kafanya nini watu hawawezi kumchukia! Kwahiyo wanaamua kunitengenezea chuki na maadui kwa watu kuwa nipo na mwanamke wangu halafu namsaliti.”Meninah “Unajua kitendo hicho hatamaye kinaniudhi naona mtu yupo na mpenzi wake halafu anamsaliti. Najua hicho ni kitendo ambacho kila mtu hakimpendezi. Kwahiyo wanaamua kunitengenezea chuki na maadui kupitia njia hiyo. Labda wana wasanii wao, sasa wanaona tukiingia kwa njia hii tutaweza kuamharibia Diamond. Ndioa siku zote nimekuwa kimya tu ila sina mahusiano na Meninah. Mie nikiwa na mtu huwa sifichi naweka wazi kabisa. Hata kama leo nimeachana na Wema nasema tu, why nifiche? Mie katika mambo yangu huwa simuogopi mtu kama ningekuwa nataka kuoa basi ninge weka wazi why nifiche?? MSIMAMO WANGU➡1.SITAONGELEA TETESI ZA HAYA MAHUSIANO SBB MAPENZI HAYAINGILIWI..2.SITAPIGA KURA WALA SITAPROMOTE UPIGAJI KURA KWA DAI MPK WEMA ATAKAPOFUNGUKA! 3.UKIMKASHFU WEMA SITAKUACHA!!�� From ma bebe @usipojipangantakupanga

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI