Thursday, August 14, 2014

"SIJAWAHI KURIDHISHWA KIMAPENZI (KUFIKISHWA KILELENI) NA MWANAUME YEYOTE TANGU NIANZE MAPENZI" - EFRANCIYA MANGII

STAA  wa  filamu  ambaye  anashika  nafasi  ya  kwanza  kwa  kufungasha  Tanzania  nzima, Efranciya  Mangii  ameibuka  na  kupasua  jipu  kuwa licha  ya  kuzalishwa  mtoto  mmoja  lakini  hakuna  mwanaume  aliyewahi  kumridhisha  kimahaba (kumfikisha kileleni).
Akiteta  na  Mpekuzi  wetu  jijini Dar es Salaam, Efranciya  ambaye  amewahi  kukumbwa  na  skendo  ya  kujihusisha  na  mapenzi  ya  jinsia  moja kwa wanawake (Usagaji )   alisema  kila  mwanaume  anayekuwa  naye  hamfikishi  popote….
"Sijawahi  na  bado  siamini  kama  naweza  kupata  mwanaume  anayeweza  kunifikisha  kileleni  na  hatimaye  kunifanya  niyafurahie  mapenzi. Hata  hivyo, ntafanyaje  na  mimi  nimeumbwa  hivi?  Kikubwa  ni  kwamba  nimezaa  na ninajisikia  faraja  sana," alisema  Efranciya.
Msanii  huyo  aliyeibukia kwenye  shindano la Maisha  Plus  na  kujizolea  umaarufu  mwingi, alieleza  kwamba  hajawahi  kujihusisha  na  usagaji  na  daima  hatathubutu  kufanya hivyo.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI