TEKNOLOJIA inazidi kukua na watu hawajaridhika kabisa na kile kinachoonekana duniani kuwa ni mageuzi.
Mjasiriamali wa Marekani ambaye ni mzaliwa wa Afrika Kusini, billionaire Elon Musk ambaye amegundua teknolojia ya mwendo kazi wa hali ya juu ‘The Hyper loop’ amekuja na wazo la kuunda treni ambayo itakuwa na mwendo mara mbili ya mwendo kasi wa ndege za kawaida.
Mara tu treni hiyo itakapotengenezwa kwa teknolojia hiyo ya mwendo kasi, itakuwa na uwezo wakuondoka mara tu abiria watapokuwa ndani ya treni hiyo kwa idadi inayotakiwa bila kusubiri ratiba baalum kama ilivyo kwa treni za umeme nchini Marekani.
Elon Musk ameeleza kuwa endapo teknolojia hiyo itakubalika na kupitishwa chombo hicyho kitakuwa na uwezo wa kubeba abiria kutoka Los Angeles hadi San Francisco ndani ya nusu saa tu!! Mwendo ambao kwa kawaida ndege hutumia zaidi ya saa moja. inaweza kutoka New York hadi China kwa muda wa saa mbili tu.
Kwa maelezo ya Elon Musk, wengi wanamuona kama amechanganyikiwa na pesa hivi lakini baadhi ya engineers wanaonekana kuiamini idea yake kwa kiasi fulani hasa baada ya kuona vifaa alivyonavyo na kuelekeza jinsi itakavyofanya kazi.
0 comments:
Post a Comment