Wednesday, August 6, 2014

HATIMAYE YEMI ALADE ATUA BONGO TZ

Hayawi hayawi sasa yamekuwa! Mkali wa ngoma ya Johnny, Yemi Alade, hatimaye katua Bongo saa tano usiku, Jumanne, Agosti 5, 2014 tayari kwa kukinukisha kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini ambalo limebakiza siku chache kabla ya kutimua vumbi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Agosti 8, 2014.
Mkali wa ngoma ya Johnny kutoka nchini Nigeria, Yemi Alade.
Akipiga stori na Showbiz, mratibu wa tamasha hilo, Luqman Maloto alisema Alade anatarajiwa kutua kwa ndege ya Shirika la Kenya Airways akitokea Lagos, Nigeria na kuwataka mashabiki wa mwanamuziki huyo, kujitokeza kwa wingi kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere.
“Kama tulivyowaahidi kwamba mwaka huu kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini tunamdondosha Yemi Alade, mwanamuziki huyo atatua leo usiku tayari kwa kazi iliyomleta Bongo, kuzikonga nyoyo za mashabiki watakaohudhuria kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini na kumtafuta Johnny wake,” alisema Maloto.
Katika tamasha hilo, mbali na burudani ya nguvu kutoka kwa Yemi Alade, pia Ali Kiba atakamua shoo ya nguvu sambamba na wasanii wengine kibao wa Bongo wakiwemo Navy Kenzo (Nahreel na Aika), Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Madee, R.O.M.A Mkatoliki, Meninah, Juma Nature na kundi zima la Wanaume Halisi, mshindi wa Shindano la Amani Talen
t Search, Paschal Dominick ‘P-Plan’ na Scorpion Girls (Jini Kabula na Isabela).
 
Yemi Alade.
Maloto aliongeza: “Package ya burudani katika tamasha hilo lenye lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya kuisaidia Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), haitaishia hapo, kutakuwa na burudani kibao kama vile mpira wa miguu na ndondi ambapo mwaka huu Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba atazichapa na Mbunge wa Nzega, Hamis Kigwangala.
“Tutakuwa na mwanamuziki Khalid Chokoraa ambaye atazichapa ulingoni na Said Memba huku Bingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Thomas Mashali akizitwanga na ‘mbunge mtarajiwa’, Mada Maugo.
“Ushindani mkali pia utawekwa na mastaa wa Bongo Movie, Cloud 112 na Jacob Steven ‘JB’ ambao siku hiyo watazipiga katika pambano la raundi 4, pia kutakuwa na mechi za mpira wa miguu kati ya Wabunge Mashabiki wa Yanga dhidi ya wenzao wa Simba, timu ya Bongo Movie itapepetana na Bongo Fleva sambamba na Azam watakaokipiga dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro.”
Tamasha hilo limedhaminiwa na ampuni ya Vodacom, Pepsi, Azam TV, E FM (93.7), Clouds FM (88.5), Sycorp pamoja na Times FM (100.5).

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI