Saturday, August 2, 2014

ANNE KANSIIME, FRED OMOND NA MC PILI PILI KUTOA BURUDANI SIKU YA JUMAMOSI GOLDEN TULIP

IMG_4281
Mchekeshaji Anne Kansiime akuzungumza na vyombo vya habari kuhusiana na burudani ya vichekesho atakayoitoa kwa mashabiki wake jijini Dar.
MCHEKESHAJI Anne Kansiime anatarajiwa kutoa burudani kubwa siku ya Jumamosi (02/08/2014) kwa mashabiki wake katika ukumbi wa Golden Tulip.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Sports Lounge, mkali huyo wa kuchekesha na sanaa za majukwaani amesema mashabiki wake watarajie mambo makubwa hapo Jumamosi.
‘Hii ni mara yangu ya kwanza kuja Tanzania, hivyo mashabiki wangu watarajie burudani ambayo itaacha mbavu zao hoi, lakini pia watapata nafasi ya kujifunza vitu vingi kupitia vichekesho vyangu’ alisema Anne.
Kwa upande wake, mchekeshaji mwingine kutoka Kenya atayetoa burudani, Fred Omondi, amesema watanzania watarajie burudani kali kama lilivyo jina la burudani yenyewe, Cheka Kwa Nguvu.
‘Usiku wa Jumamosi utawakutanisha moja ya wachekeshaji mahiri barani Afrika, hivyo watanzania waje kwa wingi kushuhudia burudani hii’ alisema Fred.
IMG_4291
Mchekeshaji kutoka Kenya, Fred Omondi akilonga na wanahabari.
Naye mchekeshaji Pilipili kutoka Tanzania amesema usiku wa leo utakuwa usiku wa kukumbukwa hasa kwa vichekesho alivyowaandalia mashabiki wake.                  
Usiku wa Cheka Kwa Nguvu unaandaliwa na kituo cha Radio 5 na pia utaambatana na burudani ya muziki kutoka ODAMA Band.
Akizungumzia tukio hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Radio 5, Robert Francis amewataka wapenzi wa burudani ya vichekesho kuhudhuria kwa wingi ili wafurahie burudani waliyowaandalia.
‘Usiku wa leo ni maalumu kwa watanzania kufurahia utanzania wao, kwani kucheka ni sehemu muhimu kwa maisha ya mwanadamu’ alisema Robert.
Kansiime amejipatia umaarufu kupitia mitandao ya kijamiii ambako alianza kwa kuweka vipande vya video akiigiza kama mwanamke wa kiafrika anayekutana na changamoto mbalimbali za maisha.
Mchekeshaji huyo wa kike, ambaye pia huendesha kipindi cha “Don’t Mess With Kansiime” kwenye kituo cha Citizen TV, anatajwa kuwa mwanamke mwenye kipaji cha pekee nchini Uganda na Afrika Mashariki kwa ujumla.
IMG_4274
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Radio 5, Robert Francis akizungumza na wanahabari.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI