Sunday, August 24, 2014

ALAMA 11 ZA KUKUONESHA KUWA MPENZI WAKO SIO MWAMINIFU AU KAANZA KUCHEPUKA

Katika Jamii Ya Sasa Kumekuwa na Kusalitiana kwa Wapenzi kwa kiwango cha Juu sana, na wengine wamekuwa wakifanya usaliti huo kwa siri sana. Zifuatazo ni signs 11 za kutaka kubaini mtu mwenye tabia ya ku-cheat. 
Ishara moja pekee haiwezi kukusababishia uka fikia hatma ya kudhani mwenzi wako ni msaliti lakini pia consistence ya jambo inaweza kuwa ni ishara nyingine.

Zifuatazo ni alama 11 za Kukuonesha kuwa mpenzi wako Sio Mwaminifu.

 1. Kuongezeka kwa ghafla kwa hali ya kujipenda:
Yawezekana mpenzi wako alikuwa amezoea kuvaa kawaida, hapa simaanishi kutopendeza, na wewe ulikuwa umemzoea katika halifulani ya mavazi au mitindo mara ghafla anabadilika nakuwa mtanashati zaidi, ana badilisha mavazi, anapenda mavazi ya garama, labda alikuwa hatumii manukato lakini gafla anaanza kupenda manukato tena ya garama, anakuwa mtu wakujijali zaidi ya kawaida yake kiasi ambacho hukumzoea. Katika hali hii jaribu kuwa macho zaidi kufahamu nini kilicho sababisha mabadiliko ya gafla kiasi hicho.

2. Kuanza kuchelewa kutoka kazini mara kwa mara:
Sio kwamba kila mtu anapochelewa kutoka kazini basi anakuwa sio mwaminifu, lakini zaidi ya asilimia 75 (kutoka kwente tafiti) ya ambao wamekuwa na mahusiano nje wamekuwa wakitoa visingizio vinavyohusiana na kazi, vikao, mikutano na safari za kikazi, yamkini wewe ni shahidi wa hili. Unaweza kukuta mtu alikuwa anafanya kazi hiyo muda mrefu tu tangia muanze mapenzi yenu, mara gafla hali inabadilika, sikuhizi anachelewa sana kurudi nyumbani, na anaporudi unaweza kutegemea utamwona amechoka kimwili na hata kiakili kwa majukumu ya kazi kuhusiana na asili ya kazi anayoifanya lakini unakuta mtu wala haonyeshi kuchoka, anafuraha kama kawaida. Hali hii inapojitokeza mara kwa mara usichelewe kufungua macho na kudadisi mazingira maana yamkini ni kweli amepata kazi ya ziada ila siyo ile ya ajira unayoijua wewe.

3. Kupenda kutembea na mipira ya kinga mara kwa mara (condoms) 
Inashangaza maranyingine kusikia mpenzi mmoja anatabia ya kubeba kondom kwenye pochi yake au mfukoni kwa kisingizio kuwa anajali, cha kushangaza zaidi unakuta yuko katika mahusiano na mkewe au mumewe. Yamkini nikweli kunakujali na labda katika mahusiano yenu hili sio la kushtua kwasababu mnajali afya zenu au mnatumia kondomu kwa sababu zaidi ya moja, lakini inakuwaje pale unapogundua kuwa ile kondom uliyokuwa unaiona haipo tena na yamkini wewe hukuhusika katika kuitumia.

4. Mazingira tatanishi ya simu:
Inawezekana mpenzi wako sio mtu wa kupokea simu au kupiga simu sana, na hivi ndiyo ulivyomzoea, mara gafla simu zinaanza kumiminika mpaka mida ya usiku. Yamkini pia alikuwa yuko huru hata simu yake inapolia waweza ichukua na kumpatia lakini gafla anakuwa na hofu kubwa na kuificha simu yake, nimeongea na wengine ambao wanakwenda na simu hadi bafuni isije ikasikika. Wengine wameanza kuondoa milio katika simu zao wakati haikuwa kawaida yao, wengine wamegundua kila mbinu ya kuweka namba ya siri (password) ngumu hadi mwenyewe anashindwa kuikumbuka wakati mwingine, wako ambao simu zao zikipigwa hawawezi kupokea na kuongea kwa uhuru kama kawaida, ataondoka na kujitenga pembeni akijifanya anaongea kiuaminifu kabisa lakini mtu uliyempenda na umkamzoea unaweza kugundua uhalisi wa anachokiongea kwenye simu na jinsia ya anayeongea naye kwa kumuangalia usoni tu. Yamkini mpenzi wako amepigiwa simu na kwasababu hakuwepo karibu ukaipokea, na mara mpigaji wa simu anapogundua aliyepokea sio mwenye simu anakata simu hiyo gafla, au gafla unagundua kila simu inayopigwa kwenye simu ya mpenzi wako haionyeshi namba au haionyeshi jina. Mazingira kama haya yanapozidi basi jaribu kuchukuwa hatua, yawezekana kuna mvamizi tayari katika mahusiano yenu.

5. Harufu ambazo hujazizoea:
Kwa kuwa wapendanao huwa wamezoeana,maranyingi hata aina ya manukato mmoja anayotumia yanakuwa yanajulikana kwa mwenzake, hata kama mmoja hajui jina la manukato anayotumia mpenzi wake lakini basi atajua walau jinsi yanavyonukia. Sasa hembu fikiri unamkuta mpenzi wako ametokea na anaharufu ya tofauti kabisa na uliyoizoea, yamkini umeisikia harufu hiyo akiwa amerudi toka kazini wakati asubuhi alipoondoka alikuwa na harufu ile uliyoizoea. Najua hali hii inaweza kuwa na sababu zinazoeleweka lakini maranyingine ni ishara ya kuashiria kutokuwepo na uaminifu baina ya mpenzi mmoja. Maranyingine sio harufu bali michubuko katika maeneo fulani ya mwili ambayo hayana maelezo fasaha yalikotokea, iko michubuko mingine ambayo inajieleza na kutia shaka zaidi, yawezekana, ni mpenzi wa kiume lakini unamkuta na ishara za rangi ya midomo (lip sick) kwenye nguo au mwilini, sidhani kama na hapa bado maelezo yake yataingia akilini kiurahisi.

6. Tabia za kuanza kukufuatilia sana au hata kukuganda:
Nimeshawahi kuwa na mazungumzo na watu wajinsia ya kike waliokuwa kwenye mahusiano ambapo wanaume wao walikuwa hawawaachi, watawapeleka kila wanakotaka, nakutoruhusu mazingira ya wapenzi hawa wakike kuwa huru kufanya mambo yao wenyewe, wengine waliitafsiri hali hii kama penzi kubwa sana, yuko aliyeniambia “mpenzi wangu ananipenda sana, yani hawezi niacha mwenyewe, kila sehemu anataka niende nae” baada ya muda mtu huyu aligundua kuwa ile ilikuwa ni ujanja wa kuficha uhalisi wake na kuzuia mazingira ya mpenzi wake wa kike kugundua au kupewa taarifa za tabia zake, na kwa muda mrefu hakugundua mpaka siku alipo pata tarifa za ukweli na ukawa mwisho wa mahusiano yao, tena mwisho wenye uchungu sana. Kuwa macho sana na tabia za mpenzi wako kukuchunguza sana unapotoka, ulipokuwa, ulikuwa nanani, mlifanya nini, nani mwingine alikuwepo, unaenda wapi, kwa muda gani. Yawezekana yote hii ni hali ya kujilinda au kujihisi mdhambi (guilty conscious) inayomsumbua.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI