Thursday, July 3, 2014

MATATIZO YA NDOA YA BEYONCE YAMFANYA ABADILI MISTARI YA WIMBO WAKE AKIWA JUKWAANI

Beyonce1
NDOA ya wanamuziki mastaa nchini Marekani Beyonce na Jay Z imekuwa katika hekaheka kubwa, ambapo mastaa hao wamekuwa wakipambana na uvumi kuwa sasa ndoa yao iko juu ya mawe kutokana na matatizo makubwa yanayoendelea tangu kusambaa kwa video ikimuonyesha dada wa Beyonce Solange akimshambulia Jay Z.
beeyonce
Na sasa Beyonce amezidi kupalilia moto zaidi kuhusiana na uvumi huo baada ya kubadilisha mistari kwenye wimbo wake kuhusu usaliti wakati akiwa jukwaani aki “perfom” kwenye ziara ya muziki na mume wake ya On The Run mjini Ohio.
Nyota huyo wa muziki wa R&B amesema kuwa Jay Z anaweza kuwa sio mwaminifu wakati akiimba wimbo wake uliotoka mwaka 2008, Resentment, ili kuendana na matukio yanayoendelea katika mahusiano yake na mumewe
Imekuwa ikivumishwa kuwa Jay Z yupo katika mahusiano ya nje ya ndoa na mwanamuziki Mya wakati wote si Jay wala Mya aliyejibu tuhuma hizo ambapo mashabiki wameendelea kuwafutilia kwa karibu hasa muziki wa Beyonce.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI