Wachezaji wa Azam Fc, wakishangilia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya city katika mchezo wao wa Ligi Kuu uliochezwa jana Jijini Mbeya na kutangaza ubingwa rasmi kwa kufikisha jumla ya Pointi 59 wakiwaacha Yanga ambao nao pia waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya JKT Orjolo walicheza jana jijini Arusha na kufikisha jumla ya Pointi 55 huku wakiwa wamesalia na mchezo mmoja dhidi yao na Simba utakaochezwa Aprili 19, ambao hata wakishinda hawataweza kufikia pointi za wapinzani wao katika mbio hizo Azam, ambao nao pia wamesalia na mchezo mmoja ambao hata wakishinda au kushinda hauna faida wala hasara kwao.
BAADA ya Azam kufanikiwa kutwaa taji la ubingwa jana jijini Mbeya kwa kuwalaza wenyeji wao Mbeya City, imeweka rekodi ya kuwa klabu ya tisa kunyakua taji hilo nchini tangu mwaka 1965.
Azam imetwaa ubingwa huo ikiwa na jumla ya Pointi 59 ikiwa imecheza michezo 25, huku wapinzani wao katika mbio hizo, Yanga wakibaki nafasi ya pili baada kuwabamiza Oljoro JKT mabao 2-1 katika mchezo wao uliopigwa kwenye Uwanja wa Sheikh AMri Abeid jijini Arusha na kufikisha jumla ya Pointi 55.
Azam waliweza kushika nafasi ya pili misimu miwili mfululizo nyuma ya Simba na Yanga, ambapo msimu huu wameonyesha uchu wa kuitamani na kumudu kuiwania vyema nafasi ya kwanza na hatimaye kufanikiwa.
Ukiondoa Yanga na Simba walionyakua mataji mara nyingi, Azam itaingia kwenye orodha ya walionyakua ubingwa huo ikifuata nyayo za Cosmopolitan iliyofanya hivyo kwa mara ya kwanza mwaka 1967.
Baada ya Cosmo waliofuata walikuwa ni Mseto ya Morogoro waliofanya hivyo mwaka 1975, kisha Pan Africans iliyoweka rekodi mwaka 1982, ikafuatiwa na Tukuyu Stars iliyonyakua mwaka 1986 na kufuatiwa na Wagosi wa Kaya, Coastal Union mwaka 1988.
Klabu ya Mtibwa Sugar ilikuja kuweka rekodi ya kunyakua taji hilo la Ligi Kuu misimu miwili mfululizo mwaka 1999 na 2000 kabla ya Simba na Yanga kupokezana taji hilo tangu hapo hadi msimu huu ambapo inaelekea wazi Azam wanaingia kwenye orodha hiyo.
Azam imeweka rekodi hiyo ya kuwa timu ya tisa kunyakua taji hilo na kuisimamisha Yanga iliyoshikilia taji hilo la 24, ikiongoza orodha ya klabu zilizonyakua mara nyingi ikifuatiwa na Simba iliyotwaa mara 18.
ORODHA KAMILI YA MABINGWA WA LIGI KUU TANGU 1965-
1965 Sunderland (Simba)
1966 Sunderland
1967 Cosmopolitan
1968 Yanga
1969 Yanga
1970 Yanga
1971 Yanga
1972 Yanga
1973 Simba
1974 Yanga
1975 Mseto
1976 Simba
1977 Simba
1978 Simba
1979 Simba
1980 Simba
1981 Yanga
1982 Pan Africans
1983 Yanga
1984 Simba
1985 Yanga
1986 Tukuyu Stars
1987 Yanga
1988 Coastal Union
1989 Yanga
1990 Simba
1991 Yanga
1992 Yanga
1993 Yanga
1994 Simba
1995 Simba
1996 Yanga
1997 Yanga
1998 Yanga
1999 Mtibwa Sugar
2000 Mtibwa Sugar
2001 Simba
2002 Yanga
2003 Simba
2004 Simba
2005 Yanga
2006 Yanga
2007 Simba
2007/08 Yanga
2000-09 Yanga
2009-10 Simba SC
2010-11 Yanga
2011-12 Simba SC
2012-13 Yanga
2013-14 Azam Fc
0 comments:
Post a Comment