Monday, March 31, 2014

TUNDU LISSU AWA NA WAKATI MGUMU SINGIDA

Mwenyekiti wa mkutano wa wazazi/walezi wa shule sekondari kata ya Unyahati jimbo la Singida mashariki na diwani wa kata hiyo, Abel Richard Suri, (wa pili kushoto) akisisitiza jambo kwenye huo uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya sekondari Unyahati.Wa kwanza kushoto ni mkuu wa shule ya Unyahati sekondari, Mkhai Marco.
.ni wanachama wa CCM na Chadema wazika rasmi sera ya kutochangia maendeleo
.iiasisiwa na Mbunge wa Singida mashariki, Tundu Lissu
Na Nathaniel Limu, Ikungi
WANACHAMA wa CHADEMA na CCM kata ya Unyahati jimbo la Singida mashariki kwa pamoja wameazimia ‘kuzika rasmi’ sera ya wananchi kugoma kuchangia miradi ya maendeleo kwa madai kwamba inarudisha nyuma maendeleo ya kata hiyo.
Sera hiyo inadaiwa kuasisiwa na Bunge (CHADEMA) wa jimbo hilo la Singida Mashariki, Tundu Lissu.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na wanaCCM, CHADEMA na wakazi wengine wa kata hiyo wapatao zaidi ya 150, Diwani kwa kata hiyo, Abel Suri amesema sera ya kugoma kuchangia maendeleo ikiwemo sekta ya elimu imedumaza kwa kiasi kikubwa maendeleo ya kata hiyo.
Akitoa mfano hai,amesema kuwa kuanzia mwaka 2011 hadi sasa, zaidi ya shilingi 75 milioni zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za kuishi walimu wa sekondari ya Unyahati, hazikutolewa kwa sababu wananchi wamegoma kuchangia na kushiriki ujenzi wake.
Mjumbe wa mkutano wa wazazi/walezi wa wanafunzi wa shule ya sekondari Unyahati jimbo la Singida mashariki, akishiriki kujadili mada/changamoto zinazoikabili shule hiyo, ikiwemo ya uhaba mkubwa wa vyoo.
“Vivyo hivyo kwa upande wa ujenzi wa maabara tatu, hali ni mbaya zaidi tumekuwa tukitengewa zaidi ya shilingi 210 milioni, lakini hatuzipati kwa sababu tumeshindwa kukidhi vigezo ambavyo vinavyohitajika ambavyo ni kujenga boma la vyumba hivyo”,amesema kwa masikitiko.
Suri amesema fedha zinazotengwa na serikali kwa maendeleo ya jimbo la Singida mashariki zote zimekuwa zikipelekwa jimbo la Singida kaskazini ambako wananchi wake wanachangia na kushiriki kikamilifu utekelezaji wa miradi yao ya maendeleo.
“Tumekubali kudanganywa tumeiachia serikali itufanyie kila kitu nadhani kila mmoja wetu ni shuhuda mzuri kwamba serikali haina uwezo huo tumedanganyika na sasa tunashuhudia kudumaa kwa maendeleo ya kata yetu”,amesema.
Baadhi ya wazazi/walezi wa shule ya sekondari Unyahati jimbo la Singida mashariki,wakifuatilia majadiliano juu ya changamoto zinazoikabili shule hiyo.
Akifafanua zaidi, amesema mfano hai ni shule ya sekondari ya Unyahati ambayo inakabiliwa na changamoto nyingi, ikiwemo ya uhaba mkubwa wa vyoo na nyumba za kuishi walimu.
“Hivi sasa wakija maafisa afya,shule hii inafungwa. Shule haina jengo la utawala inatumia vyumba za madarasa kuwa ni ofisi za walimu haina nyumba hata moja ya kuishi walimu, walimu wote wamepanga Ikungi kitendo kinachosababisha watembee kilomita nane kwenda na kurudi shuleni”,amesema.
Baada ya maneno hayo, wazazi/walezi kwa kauli moja walikubaliana kufufua moyo uliokuwepo na kuchangia maendeleo yao na kwa kuanzia wataanza na kuchangia na kushiriki ujenzi wa vyoo vya shule yao na kisha baadaye wajenge nyumba za kutosha walimu kuishi katika maeneo ya kituo chao cha kazi.
Kaimu mkuu wa shule ya sekondari ya Unyahati jimbo la Singida mashariki, Mboya David, akikagua choo cha nyasi kinachotumiwa na wanafunzi wa shule hiyo.Imedaiwa wanafunzi wengine hujisaidia vichakani kitendo kinachohatarisha maisha yao kutokana kuwepo na nyoka wengi.
(Picha na Nathaniel Limu).

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI