Wednesday, November 7, 2012

UCHAGUZI MAREKANI - OBAMA ASHINDA!

''Naamini tunauwezo wa kuijenga Marekani katika yote tuliyo yaanzisha na tunayoendelea nayo ambapo tunapigana dhidi ya upatikanaji wa Ajira, na usalama wa watu wetu wa tabaka la kati. Naamini tunauwezo wa kuzitekeleza ahadi zilizoahidiwa na viongozi wetu waliopita, kama uko tayari kufanya kazi kwa juhudi, haijalishi we ni nani, unatokea wapi, unaonekanaje au unapenda sehemu gani? Haijalishi kama wewe ni mweusi au mweupe, mhispania au muasia, Mmarekani asilia, Kijana au mzee, tajiri au maskini, unauwezo au Mlemavu, Shoga au Vinginevyo, Unauwezo wa kufanya lolote kama utaamua kujaribu''


Na Aziza Gulu, Frank Mavura

Rais wa Maerkani Barack Obama amewashukuru wamarekani kwa kuonesha imani juu ya uongozi wake na kumpa ridhaa ya kuongoza tena taifa hilo kwa  miaka minne ijayo.
Katika hotuba yake baada ya kutangazwa kushinda rais Obama amesema kuwa kwa sasa anarejea ikulu akiwa na malengo thabiti na mwenye ari zaidi ya awali kwa lengo la kuwatumikia raia wa taifa hilo.

Raia wa Marekani wakiwa wamejitokeza kufurahia ushindi wa Rais Barak Obama kutoka Democratic
Aidha rais Obama amemshukuru mpinzani wake Mitt Romney kwa kampeni zenye ushindani na kwamba ataendeleza ushirikiano na gavana huyo ili kuliwezesha taifa hilo kusonga mbele kwa manufaa ya wamarekani wote. Wakati huo huo Romney amempongeza Obama kwa ushindi wake.

Rais Barack Obama akimpa mkono na mpinzani wake Mitt Romney (Picha: AFP)
Mshindi wa kiti cha Urais, Barack Obama akiwa na mkewe Michelle Obama na watoto wake Sasha na Maria wakiwa katika jukwaa baada ya Rais Obama kutangazwa mshindi tena kuiongoza Marekani kwa Kipindi kingine cha miaka Minne dhidi ya mpinzani wake kutoka Republican Mitt Romney. (Picha: Jewel Samad AFP)


Baadhi ya raia wa Marekani wakiwa wameshikilia bango lililoandikwa TUMESHINDA!!!


Rais Obama amemshinda mpinzani wake Mitt Romney ambaye amepata kura 203 kutoka katika majimbo 13 na  kwa wingi wa kura za majimbo amepata jumla ya kura 206 dhidi ya kura 303 alizopata Romney,ambaye hata hivyo ameshinda Obama kwa kura za wananchi kwa asilimia 50 ya kura huku Obama akiambulia asilimia 49.

Swali ni kwamba watanzania tunajifunza nini kutokana na harakati za kampeni zilizofanyika hatimaye chaguzi zilizofanywa na wenzetu huko nchini Marekani, ambapo uchaguzi ulienda vizuri kabisa na hatimaye Rais Barack Obama kushinda kiti cha Urais kwa awamu nyingine tena?

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI